KIPI KINASABABISHA MVURUGIKO WA SIKU ZA HEDHI KWA WANAWAKE?

0:00

9 / 100

AFYA

🌟 Kuelewa Mvurugiko wa Siku za Hedhi kwa Wasichana 🌟

Hizi hapa ni baadhi ya sababu zinazoweza kupelekea mvurugiko wa siku za hedhi:

💠 Umri:

Wanawake wenye umri wa miaka 40 na kuendelea wapo kwenye hatari ya kuwa na mvurugiko wa siku za hedhi kutokana na upungufu wa ufanyaji kazi wa ovari katika kuzalisha mayai yenye ubora mzuri.
💠 Mazoezi Makali: Ingawa mazoezi kwa ujumla yanafaa kwa afya yako, mazoezi makali yanaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kubadilika badilika .

💠 Msongo wa Mawazo:

Msongo wa mawazo huathiri utendaji kazi wa mwili na kupelekea mvurugiko wa siku za hedhi.

💠 Maambukizi ya Magonjwa:

Hali duni ya afya kutokana na maambukizi kama virusi inaweza kusababisha mvurugiko wa siku za hedhi.
💠 Mabadiliko katika Mtindo wa Maisha:

Kupungua au kuongezeka uzito kunaweza kuathiri mzunguko wa hedhi.
💠 Saratani ya Mfuko wa kizazi:

Msichana mwenye aina hii ya saratani anaweza kupata mvurugiko katika siku zake za hedhi.

💠 Matumizi ya Mpango wa Uzazi kwa njia ya homoni:

Matumizi yasiyo sahihi ya vidonge vya mpangilio wa uzazi yanaweza kupelekea mvurugiko wa siku za hedhi.
Hizo ni baadhi ya sababu kati ya nyingi zinazoweza kusababisha mvurugiko wa siku za hedhi. Kufanya uratibu kamili na kujua hali ya usalama wa mzunguko wa hedhi, ni vizuri kupata mazungumzo binafsi na daktari ili kupata msaada wa karibu na kufuata njia sahihi za kuwa salama wakati wa hedhi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAAJABU YA MANCHESTER CITY KWENYE LIGI YA...
MICHEZO
See also  Mfanyakazi wa Ndani Aliyemkata Shingo Mtoto Akamatwa Dar
Manchester City ikicheza ,imetokea nyuma na kushinda licha ya...
Read more
DON 3 KUACHILIWA BILA MKALI SHAHRUKH KHAN...
Nyota Wetu Hii ni habari kama isiyopendeza kwa mashabiki wa nguli...
Read more
Fulham have reached an agreement with Arsenal...
Smith Rowe is a club record signing for Fulham and...
Read more
Bayern's Kompany happy with performance after 3-3...
Bayern Munich conceded a late equaliser for a 3-3 draw...
Read more
Emeka Anyaoku Calls For new constitution for...
Former Secretary General of the Commonwealth, Chief Emeka Anyaoku, was...
Read more

Leave a Reply