WANAODAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKAHABA KULIPWA MABILIONI

0:00

10 / 100

HABARI KUU

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC) Hassan Bomboko ametakiwa kulipa kiasi cha Sh. Bil 36 kutokana na sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba.

Suala hilo limechukua sura mpya, baada ya DC huyo kupewa notisi ya kuwalipa kiasi hicho wanawake hao.

Notisi hiyo ya wiki mbili imeanza jana Alhamisi, Juni 20, 2024 na inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai kudhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa siku tano kinyume na sheria.

Notisi hiyo imeandikwa na wakili wao kutoka tasisi ya Stalwart, Peter Madeleka ambaye amethibitisha kwamba tayari wameshaiwasilisha kwa kiongozi huyo.

DC Bomboko alisema alikuwa hajapokea notisi hiyo inayoelezwa amepelekewa. ” Sijapokea hiyo notisi. Muulizeni vizuri.” Alipotafutwa tena jioni hakupatikana.

Hivi karibuni iliwakamata ‘makahaba’ hao Ubungo, River Side na Sinza, bado inavuta hisia za wengi mitandaoni wakieleza inaingilia faragha za watu na inakiuka haki za binadamu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU SINGAPORE KUKATAA KUANDAA MICHEZO YA JUMUIYA...
MICHEZO Singapore imekataa kuandaa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya...
Read more
DRC army says it stopped attempted coup...
LATEST NEWS The leader of an attempted coup on Sunday...
Read more
15 reasons why you should visit the...
Rich Cultural Heritage: Experience the unique cultural practices and traditions...
Read more
Kenyan Youth Movement, Gen Z, Enjoys Widespread...
A recent survey conducted by the Trends and Insights for...
Read more
VYAMA VYAONYESHA SHAKA UCHAGUZI WA HURU NA...
MAGAZETI
See also  Rais Samia agawa zawadi ya Tausi
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply