RAIS WA GUINEA BISSAU KUZURU TANZANIA KIKAZI

0:00

10 / 100

HABARI KUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam ambaye atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru. Ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru.

Wakati wa ziara hiyo, Marais hao wawili wanatarajia kuongoza mazungumzo rasmi ya kiserikali kati ya Tanzania na Guinea-Bissau na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano (General Framework Agreement) ambao utaongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Mbali ya mazungumzo na Rais Samia, Rais Embaló atatembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Makao Makuu ya Sekretarieti ya Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) yaliyopo hapa nchini, ambapo yeye ni Mwenyekiti wa ALMA.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WIZKID ATAJA SABABU YA KUKATAA MZIKI WA...
NYOTA WETU Msanii wa Afrobeats kutoka Nigeria Wizkid amewashangaza wengi...
Read more
ONANA KUIKOSA GUINEA AFRICON
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
YANGA KUMALIZA KAZI LEO CAFCL? ...
Magazeti Magazeti kwa njia ya picha,
See also  KEPA ARRIZABALAGA AKOSA NAMBA REAL MADRID
Read more
CAF YATOA MAELEKEZO HAYA KWA SIMBA
MASTORI CAF imeielekeza klabu ya Simba SC kuondoa neno "MO...
Read more
VICTOR OSIMHEN KUAMIA LIGI YA ENGLAND
MICHEZO Licha ya kipaumbele cha Victor Osimhen msimu wa joto...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply