TEC YAPATA SAFU MPYA YA UONGOZI

0:00

7 / 100

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limemchagua Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Wolfgang Pisa kuwa Rais wake baada ya uongozi uliopita kumaliza muda wake wa kikatiba.

Aidha, TEC imemchagua Askofu wa Jimbo la Mpanda, Eusebius Nzigilwa kuwa Makamu wa Rais.

Askofu Wolfgang Pisa alipata elimu yake Maua Seminary akasoma pia UDSM, Zambia na Marekani. Kisha kuliongoza Shirika la Wafransisko Wakupuchini Tanzania. Pia aliwahi kufundisha chuo cha SAUT tawi la Arusha.


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limemchaga Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi Mhashamu Wolfgang Pisa, OFMCap kuwa Rais mpya wa Baraza hilo, huku Mhashamu Eusebius Nzigilwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda akichaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Baraza hilo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Juni 21, 2024 Baraza hilo pia limemchagua Padri Dakta Charles Kitima kuwa Katibu Mkuu wa Baraza hilo huku Padri Chesco Msaga akiwa Naibu Katibu Mkuu.
Taarifa hiyo imetolewa mapema leo Juni 22, 2024 na Rais aliyemaliza muda wake Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani kwa Mungu kwa kupata uongozi mpya, iliyoadhimishwa katika Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, Makao Makuu ya TEC, Kurasini Dar Es Salaam.
Askofu Mkuu Nyaisonga kwenye homilia yake amempongeza Rais mpya Mhashamu Pisa na safu yake kwa kuaminiwa na Baraza hilo huku akiwashukuru pia watendaji wote wa Sekretarieti, ambapo ametumia pia fursa hiyo kuomba radhi pale palipotokea kasoro katika uongozi wake.
Kwa upande wake Rais mpya Askofu Pisa amemshukuru Mungu na Maaskofu kwa kumpa jukumu hilo yeye na wenzake na kuongeza kuwa wapo tayari kutekeleza, ambapo amekazia kwamba kiongozi wao mkuu ni Yesu Kristo na wao ni watumishi, ambao kwa njia ya Sala na maombezi ya Kanisa wanaamini yote yatawezekana.
Aidha amempongeza na kumshukuru Askofu Mkuu Nyaisonga na Makamu wake Askofu Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki Geita kwa kazi kubwa waliyoifanya, ambapo ameahidi kuendeleza pale walipoishia huku akiomba ushirikiano na mwongozo kila watakapobisha hodi.
Wengine waliochaguliwa kuingia katika Kamati Kuu {Permanent Council} ni Wenyeviti wa Kurugenzi mbalimbali akiwemo Askofu Mkuu Isaack Amani{Uchungaji}, Askofu Anthony Lagwen{Fedha}, Askofu Augustino Shao ALCP/OSS{Ukaguzi}, Askofu Henry Mchamungu {Sheria}, Askofu Eusebius Nzigilwa{Mawasiliano} na Viogozi wengine waliochaguliwa wataendelea kutangazwa baadaye.
Viongozi wote wapya wameapishwa leo Juni 22, 2024 katika Adhimisho la Misa Takatifu na Mwanasheria wa Baraza hilo Padri Daniel Dulle.

See also  IBRAHIM IMORO MBIONI KUTUA TIMU HII YA KARIAKOO
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Murulle Youth Emphasize Family Unity at Nairobi...
Learnered youth from the Murulle community, particularly from the Ali...
Read more
Wanajeshi waliokimbia vita wahukumiwa kunyongwa
HABARI KUU Mahakama ya kijeshi katika mji wa Goma huko...
Read more
RAIS ALI HASSAN MWINYI AFARIKI DUNIA
HABARI KUU Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Read more
Hardship: Tinubu not aware Nigerians are hungry,...
Senate Chief Whip, Ali Ndume, has said that President Bola...
Read more
"NILITOLEWA USICHANA WANGU MARA MBILI" Wastara
NYOTA WETU "Mimi nilitolewa bikra mara mbili, mara ya kwanza...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply