HABARI KUU
Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki (EFD) na ritani za kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia Mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Dar es salaam wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya Wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
“Wafanyabiashara walionesha changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususani Bandarini ambayo inasababisha makadirio ya kodi ambayo sio sahihi lakini pili ukokotoaji wa kiwango cha kodi wanacholipa, tatu ni uwepo wa Machinga katika maduka wanayouza na nne suala la kamatakamata inayoendeshwa na TRA na nne walionesha changamoto ya muswada wa sheria ya fedha” ——— Profesa Mkumbo.
“Bado ya majadiliano ya kina tunakubaliana kuanzia July 01,2024 TRA itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri katika kuhakisha Wafanyabiashara wanapata makadirio sahihi kwa maana ya mfumo wa stakabadhi na marisiti yake”
“Suala la pili TRA inasitisha oparesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya mapato hususani katika suala la nyaraka, kuhusu ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria na sisi kaam Serikali tumelichukua ili kuboresha zaidi mfumo wa ukokotoaji wa kodi hususani Bandarini”
Profesa Mkumbo.