Bunge lamshushia Rungu Zito Mbunge LUHAGA MPINA

0:00

11 / 100

HABARI KUU

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amefungiwa kuhudhuria vikao 14 vya Bunge kuanzia leo Juni 24, 2024 baada ya ‘kutiwa hatiani’ kwa kosa kukiuka kanuni za Bunge, kudharau mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge.

Mpina amepewa adhabu hiyo baada ya wabunge kuchangia hoja ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo baada ya uchunguzi wake ilipendekeza mbunge huyo apewe adhabu ya kutohudhuria vikao visivyopungua 10.

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na bunge kufanya hivyo.

Mbunge huyo aliwasilisha ushahidi baada ya kusema bungeni kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kiwango cha upungufu wa sukari nchini, kwamba kampuni zilizopewa vibali vya kuagiza sukari hazikuingiza sukari nchini na kwamba waziri alikataa kufanya kikao na wadau wa sukari.

Kufuatia adhabu hiyo, Mpina hatohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia, hatohudhuria Bunge la Septemba na ataanza kushiriki kikao cha pili cha Bunge la Novemba mwaka huu.

Baada ya kupewa adhabu hiyo, spika alimtaka Mpina ambaye alikuwa ndani ya ukumbi wa Bunge kutoka ndani ya ukumbi, ikiwa ni mwanzo wa kutumikia adhabu yake.

Wakati huo huo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imesema uchunguzi wake umebaini kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe hakusema uongo bungeni kama ambavyo ilidaiwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina.

Hayo yameelezwa bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Mjini, Ally Makoa wakati akiwasilisha maoni ya kamati juu ya ushahidi wa Mpina kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilipotosha Bunge kwa kusema uongo.

See also  SABABU ZA YANGA KUWEKA KAMBI YAKE URUSI

Juni 4 mwaka huu wakati Waziri Bashe akitoa ufafanuzi kuhusu suala la upungufu wa sukari nchini, Mpina alisimama bungeni na kusema kwamba maelezo aliyoyatoa waziri kuhusu kiasi cha upungufu wa sukari, na maelezo kwamba hadi Januari mwaka huu hakuna kampuni iliyopewa kibali cha kuingiza sukari kwamba ni uongo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ASKOFU AJINYONGA KISA MADENI NA MGOGORO
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KWANINI UNYWAJI WA MVINYO HUSABABISHA MAUMIVU YA...
MAKALA Watafiti wa Marekani wanasema wamegundua ni kwanini baadhi ya...
Read more
MR IBU AFARIKI DUNIA
MICHEZO/BURUDANI Mchekeshaji na Mwigizaji Legend wa Nollywood Nigeria John Okafor maarufu...
Read more
WILLIAM RUTO akoshwa na Maandamano atoa Ahadi...
HABARI KUU Rais wa Kenya William Ruto leo June 23,2024 amesema...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO 7 AGOSTI...
Dar es salaam Mpemzi msomaji wa Magazeti ni asubuhi nyingine...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply