MUSUKUMA amshukia Luhaga Mpina Bungeni

0:00

9 / 100

Mbunge wa Geita, Joseph kasheku maarufu Musukuma amelishauri Bunge kumfanyia uchunguzi wa afya ya akili Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiamini huenda hayuko sawa.

Musukuma ametoa ushauri huo 24 June 2024 akisema kuwa matendo ambayo Mpina aliyafanya akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi yanamfuata hadi leo akisema kuwa aliwasababishia watu wengi maumivu.

Musukuma ametoa pendekezo hilo wakati akichangia hoja ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu uchunguzi wa kamati juu ya tuhuma dhidi ya Mpina ya kudharau mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge.
Hapo jana Mbunge Mpina amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 baada ya ‘kutiwa hatiani’ kwa kosa kukiuka kanuni za Bunge, kudharau mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge.

Mpina amepewa adhabu hiyo baada ya wabunge kuchangia hoja ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo baada ya uchunguzi wake ilipendekeza mbunge huyo apewe adhabu ya kutohudhuria vikao visivyopungua 10.

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na bunge kufanya hivyo.

Mbunge huyo aliwasilisha ushahidi baada ya kusema bungeni kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kiwango cha upungufu wa sukari nchini, kwamba kampuni zilizopewa vibali vya kuagiza sukari hazikuingiza sukari nchini na kwamba waziri alikataa kufanya kikao na wadau wa sukari.

Kufuatia adhabu hiyo, Mpina hatohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia, hatohudhuria Bunge la Septemba na ataanza kushiriki kikao cha pili cha Bunge la Novemba mwaka huu.

See also  Baada ya kuondolewa katika Uongozi wa Chama cha CNL katika Mkutano uliofanyika mkoani Ngozi Kaskazini mwa Burundi, Mhe.Agathon Rwasa amerejea nchini baada ya kuwa nje ya nchi kikazi.Mbunge Agathon Rwasa amepokelewa na familia na wafuasi wake katika chama cha CNL.Nafasi ya Kiongozi huyo wa zamani wa kundi la waasi mwenye umri wa miaka 60 imechukuliwa na Nestor Girukwishaka.Chama cha CNL ambacho kilianzishwa mwaka wa 2019, kilisimamishwa mwaka jana na serikali ya Burundi ikikituhumu kutotii sheria na kuhataraisha usalama wa ndani wa nchi.

Baada ya kupewa adhabu hiyo, spika alimtaka Mpina ambaye alikuwa ndani ya ukumbi wa Bunge kutoka ndani ya ukumbi, ikiwa ni mwanzo wa kutumikia adhabu yake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Contract extension talks have begun between Liverpool's...
Liverpool captain Virgil van Dijk has said formal discussions over...
Read more
Pastor Jeremiah Fufeyin files lawsuit against verydarkman...
The legal storm surrounding Verydarkman escalates as Pastor Jeremiah Fufeyin...
Read more
Ten Hag rejects Ronaldo criticism over ambition
Manchester United manager Erik ten Hag has dismissed Cristiano Ronaldo's...
Read more
Blord spotted having a great time and...
Linus Williams, a prominent figure in the Cryptocurrency industry and...
Read more
NASTY C TIME IS OVER
CELEBRITIES "At some point in time I was the best...
Read more

Leave a Reply