Kwanini JUDITH SUMINWA Hataki Suluhu na PAUL KAGAME?

0:00

9 / 100

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka amesema kwamba Serikali ya Kinshasa haitaki mazungumzo na Rwanda kwa sababu inaituhumu kuwasaidia Waasi wa Kundi la M 23 huko Mashariki ya nchi yake.

Alipoitembelea kambi ya wakimbizi karibu na Goma AlhamisI, Tuluka ametoa wito kwa washirika wakuu wa Congo kuchukua hatua kali na vikwazo dhidi ya Kigali.

Alhamisi hiyo Rais wa Angola Joao Lourenco akiwa katika ziara huko Ivory Coast amesema kwamba mazungumzo yanaendelea katika kiwango cha mawaziri kwa lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda na DRC kwa haraka iwezekanavyo ili kukubaliana juu ya kupatikana amani ya kudumu Mashariki ya Congo.

Angola imekuwa ikijaribu kupatanisha nchi hizo mbili kutokana na ugomvi katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini ambako waasi wa M 23 wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipigana na Jeshi la Serikali tangu mwishoni mwa 2021.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Create a DIY Rotating Irrigation System with...
IntroductionRecycling for Gardening: Learn how to create a rotating irrigation...
Read more
SABABU YA WAZIRI PAULINE GEKUL KUFUTWA KAZI...
HABARI KUU Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua...
Read more
PISTORIUS AACHIWA BAADA YA MIAKA 11 ...
NYOTA WETU. Mwanariadha wa zamani wa mbio fupi . Oscar...
Read more
DIAMOND SASA APIGWA CHINI YOUTUBE
Dar es salaam Miongoni mwa rekodi ambayo nyota wa Bongo...
Read more
WILL SMITH NDOA YAKE IMEMSHINDA ...
NYOTA WETU Muigizaji na mtangazaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Saka's injury is not serious, Arsenal boss Arteta says

Leave a Reply