Kilichosababisha Waandamanaji 39 kuuawa Kenya chatajwa

0:00

10 / 100

Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu nchini Kenya, imeripoti kuwa Jumla ya watu 39 wameuawa katika maandamano dhidi ya serikali nchini Humo, huku wanaharakati wakiongeza juhudi za kuitisha duru nyingine ya maandamano wiki hii.

“Takwimu kutoka kwa rekodi zetu zinaonyesha kuwa watu 39 wamekufa na 361 kujeruhiwa kuhusiana na maandamano ya nchi nzima,” tume hiyo ya haki za binadamu inayofadhiliwa na serikali imeeleza katika taarifa yao, na kuongeza kuwa takwimu hizo zinahusu kipindi cha kuanzia Juni 18 hadi Julai 1.

Tume hiyo imeeleza pia kuwa kuna kesi 32 “za watu waliotoweka” na waandamanaji 627 waliokamatwa.

Maandamano hayo yakiongozwa hasa na vijana, yalifanyika kwa amani kwa kiasi kikubwa, lakini yaligeuka kuwa vurugu mbaya Jumanne wakati wabunge walipopitisha mswaada wa fedha wenye utata.

Baada ya mswaada huo kupigiwa kura, umati wa watu ulishambulia jengo la bunge mjini kati Nairobi na sehemu ya jengo hilo kuchomwa huku polisi wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Maandamano mapya yameitishwa kuanzia leo Julai 2, 2024 huku Tume ikiwataka Waandamanaji walioharibu na kuchoma Miundombinu muhimu ya Serikali ikiwemo majengo ya Bunge na Maktaba ya Kitaifa kuheshimu Utawala wa Sheria wanapotumia Haki yao ya Kuandamana ili kuzuia Vifo na Vurugu


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  THE TRUTH ABOUT SEX MEN DON'T WANT YOU TO KNOW
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading