Kwanini Mahakama imemfutia Donald Trump mashitaka yanayomkabili?

0:00

12 / 100

WASHINGTON

Mahakama Kuu ya Marekani imeamua kwamba Donald Trump hawezi kushtakiwa kwa matendo ambayo yalikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba kama Rais katika uamuzi wa kihistoria unaotambua kwa mara ya kwanza aina yoyote ya kinga ya Rais dhidi ya mashtaka.

Majaji, katika uamuzi wa 6-3 ulioidhiishwa na Jaji Mkuu John Roberts, wametupilia mbali uamuzi wa mahakama ya chini ambao ulikuwa umekataa madai ya Trump ya kinga dhid ya mashtaka ya jinai ya shirikisho yanayohusiana na juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake na Rais Joe Biden katika uchaguzi wa 2020.

Majaji sita wasiopenda mabadiliko wameunga mkono uamuzi huo wa Mahakama Kuu, wakati watatu wa mrengo wa kushoto wamepinga.

“Tumehitimisha kwamba chini ya muundo wetu wa kikatiba wa kugawanya madaraka, asili ya mamlaka ya Rais inataka kwamba Rais wa zamani awe na kinga fulani dhidi ya mashtaka ya jinai kwa matendo rasmi wakati wa kipindi chake ofisini,” amesema Jaji Roberts.

Trump ni mgombea wa Chama cha Republican anayemkabili mgombea wa Democrat Rais Biden katika uchaguzi Mkuu wa Marekani Novemba 5, 2024 katika marudio ya uchaguzi wa 2020.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

FAMILIA YA GLAZER YAKATAA KUIUZA MANCHESTER UNITED...
London Wamiliki hao wa klabu hiyo ya England wanatarajiwa kufuta...
Read more
AYRA STARR SPARKS A BUZZ AS SHE...
OUR STAR 🌟 Ayra Starr sparks a buzz as she...
Read more
TANZANIA YAFUZU AFRICON MBELE YA ALGERIA ...
Michezo Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa stars" imeandika rekodi...
Read more
MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOUAWA WAKIWA MADARAKANI...
MAKALA
See also  Motsepe: Goli la Aziz Ki lilikuwa halali
Pamoja na Marais kuwa na ulinzi mkubwa lakini wapo...
Read more
ERIKA DE SOUZA VIEIRA APELEKA MAITI BENKI...
HABARI KUU Polisi nchini Brazil wanamshikilia Érika de Souza Vieira...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply