0:00
Daraja la John Magufuli (Kigongo- Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3.0 na Barabara unganishi Kilomita 1.66 linatarajiwa kuanza kutumika Disemba 30 mwaka huu likiunganisha Barabara Kuu ya Usagara- Sengerema- Geita zenye urefu wa Kilomita 90.
Daraja hilo lenye urefu wa Kilometa 3.0, upana Meta 28.45 unaojumuisha njia mbili za magari zenye upana wa meta 7.0 kila upande, njia ya maegesho ya dharura meta 2.5 kila upande.
Pia, njia za watembea kwa miguu Meta 2.5 kila upande, eneo la kati linalotenganisha uelekeo tofauti wa barabara Meta 2.45, Kingo za magari Meta 0.5 kila upande na kingo za watembea kwa miguu Meta 0.5 kila upande.
Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa kushirikiana na China Railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC – CR15G JV) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 592.6 bila VAT ya asilimia 18.
Meneja Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 88.61 dhidi ya asilimia 91.70 ya mpango kazi namba 5 ulioidhinishwa huku vifaa na mitambo ya ujenzi vilivyofika eneo la kazi hadi sasa vimefikia asilimia 99.
Mhandisi Ambrose amesema mradi huo umeshatoa jumla ya ajira 29,211 tangu kuanza kwake tarehe Februari 25, 2020 na kwamba asilimia 93.33 sawa na ajira 27,262 ni wazawa na ajira 1949 sawa na asilimia 6.67 ni wageni.
“Daraja hili likikamilika litakuwa na nyingi ikiwemo kupunguza muda wa kusafiri na uwepo wa uhakika wa usafiri masaa 24. Aidha, kuondoa msongamano wa magari uliokuwa unatokea kwenye feri, kuwa kiungo muhimu kwa Mkoa wa Mwanza na mikoa inayouzunguka pamoja na nchi jirani na pia daraja hili litakuwa ni kivutio muhimu kwa Mkoa wa Mwanza na ni nembo kwa nchi ya Tanzania.” Alisema Mhandisi Ambrose.
Amesema Daraja litakuwa na nguzo nyingine 64, ambapo 2 kati ya hizo zitakuwa umbali wa mita 100 kutoka nguzo moja hadi nguzo kuu wakati zilizobaki zitakuwa umbali wa mita 40 kutoka nguzo moja hadi nyingine na Jumla ya nguzo katika daraja lote zitakuwa ni 67.
Related Posts 📫
Conor Gallagher is likely to be sold in the summer,...
Scott McTominay is said to be close to completing his...
MICHEZO
Baada ya taarifa za kumpa mkataba wa awali Beki...
MICHEZO
Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kufanya mazungumzo na...