Mwanafunzi wa moja ya vikuo vikuu jijini Mwanza, Tumsime Mathias (21) ambaye anadaiwa kulawitiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda amesema amelazimika kusitisha masomo kwa muda kutokana na tukio ukatili wa kingono ambao anadai kutendewa na mkuu huyo wa mkoa.
Amesema hayo leo Julai 05, 2024 akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameviomba vyombo vya kutoa haki, kuhakikisha kwamba haki inatendeka ikiwemo kesi yake kufikishwa mahakamani.
Akizungumzia magumu anayopitia kufuatia tukio hilo, Tumsime amesema kwa sasa anapitia wakati mgumu hali inayomlazimu pia kuhama maeneo anayoishi akihofia usalama wake.
Sambamba na hilo, Tumsime amemuomba Rais Dkt. Suluhu Samia kumsaidia kuingilia kati suala lake hilo ili aweze kupata haki yake.
“Namuomba Rais Suluhu Samia aingilie kati kwa kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mahakamani” alisema Tumsime na kuongeza
“Suala hili lipelekwe mahakamani ili haki itendeke, kama mimi (Tumsime) nina makosa basi niadhibiwe, lakini kama sina basi mtuhumiwa achukuliwe hatua za kisheria”