Mwalimu Jela kwa Kuruhusu Mwanafunzi Kumlawiti

0:00

9 / 100

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa
Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema mwalimu huyo siku za nyuma alijenga urafiki shuleni na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa shuleni na kumtaka akamtembelee nyumbani.

Amesema mwalimu huyo alimtaka mwanafunzi huyo akamtembelee nyumbani na alipoenda alianza kumuonyesga video chafu kupitia simu janja na baadae kumtaka amuingilie kinyume na maumbile.

Baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho ndipo mwalimu akaanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule.

Baada ya vitisho hivyo mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake.

Katika hatua nyingine Bakari Katembe mwenye umri miaka 19 mkazi wa Kijiji cha Mdumbwe amehukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu.

Mtuhumiwa huyo alimlaghai mtoto huyo kwa kumununulia pipi kisha kumchukua kwenda naye nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Croatia and Argentina finalise United Cup lineup
SYDNEY, - Croatia and Argentina have taken the last two...
Read more
AL AHLY YAONDOLEWA KLABU BINGWA YA DUNIA
MICHEZO Mabingwa wa Afrika, AL AHLY wametolewa kwenye michuano...
Read more
JINSI YA KUTEKA HISIA ZA MWANAMKE KIMAPENZI...
MAPENZI Nyumba nyingi zina vilio, mateso ,maumivu na hata visasi...
Read more
Lege Miami video sparked controversy as he...
The heartwarming interactions between the well-known Nollywood actor Lege Miami...
Read more
How the Mind of Woman Works in...
Women will never tell you this, but I'll tell you...
Read more
See also  RAILA ODINGA ATAJA VIPAUMBELE AKICHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA AU

Leave a Reply