Mfahamu Rais Mpya wa Iran Masoud Pezeshkian

0:00

9 / 100

Mgombea wa Urais na mwanamageuzi Nchini Iran, Masoud Pezeshkian ameshinda uchaguzi wa Rais katika duru ya pili dhidi ya Mhafidhina Saeed Jalili.

Matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani yanaonesha kuwa Pezeshkian amepata zaidi ya kura milioni 16 na Jalili amepata kura zaidi ya milioni 13 kati ya kura milioni 30 zilizopigwa ambapo watu waliojitokeza kupiga kura walifikia asimilia 49.8 kwa mujibu wa Msemaji wa Mamlaka ya uchaguzi Mohsen Eslami.

Viongozi mbalimbali Duniani akiwemo Rais Vladmir Putin wa Urusi na uongozi wa Saudi Arabia wametuma salamu za pongezi kwa Mwanamageuzi huyo kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Iran.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Masoud Pezeshkian amewashukuru Watu wa Iran kwa kumchagua mwenye uchaguzi huo uliofanyima baada ya kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

IMF Advises Kenya to Strengthen Tax Capacity...
The International Monetary Fund (IMF) has issued a new tax...
Read more
WILLIAM RUTO KAMA MAGUFULI ...
HABARI KUU Rais wa Kenya 🇰🇪 Dkt. William Ruto amesema...
Read more
Mauricio Pochettino hana presha ndani ya Chelsea
MICHEZO Licha ya kufungwa mabao 5-0 na Arsenal juzi Jumanne...
Read more
Fahamu Sababu za Mimba Kuharibika
AFYA Mimba kuharibika ni kitendo cha mwanamke kupoteza mimba au...
Read more
KWANINI RWANDA IPO TAYARI KUINGIA VITANI NA...
Katika mahojiano maalum na FRANCE 24, Rais wa Rwanda Paul...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  AJALI ILIVYOUWA WATU 7 MOROGORO

Leave a Reply