Jinsi Unyago na Jado zinavyosaidia Kukuza na Kuendeleza Maadili

0:00

10 / 100

Imeelezwa kuwa unyago ni njia mojawapo inayosaidia kukuza na kuendeleza maadili mema ya kitanzania katika jamii ya watanzania.

Hayo yamebanishwa na mmoja wa manyakanga Bibi Pili Tamla wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya wadau wa utamaduni iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) yenye lengo la kuishirikisha jamii kutambua na kuhifadhi utamaduni wa urithi usioshikika (ICH).

Unyago ni mafunzo anayopewa binti aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea yanayohusu namna ya kuwa na maadili mema katika jamii yake. Mafunzo hayo hutolewa na watu wenye ujuzi maalumu ya kimaadili ya mahali husika kwenda kwa mabinti maarufu ‘Nyakanga’ hasa katika jamii ya Wakwere na Wadoe wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Nyakanga Pili alisema kwamba mafunzo ya unyago yamekuwa yakibadilika kutokana na maendeleo ya elimu ambapo kwa sasa hutolewa katika umri wa kuanzia miaka 18 na mara nyingi wakati wa likizo za shule.

“Wakati wa Unyago tunawafunda mabinti wawe wasafi, wawe na adabu na wasiwe waongo. Tunawafunza nidhamu na kusisitiza kuheshimu wakubwa.” Alisema Bibi Pili.

Alisisitiza kuwa kuiga mambo ya wazungu kumefanya jamii hususani kizazi cha sasa kuwa na vijana ambao hawaheshimu wakubwa na kuongezeka kwa mmonyoko wa maadili kwenye kjamii.

Kwa upande wake, Wakili Philomena Mwalongo ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya YOGE alisisitiza umuhimu wa kutengeneza maktaba ya utamaduni wa urithi usioshikika ili kuweza kurithisha mila na desturi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Mafunzo hayo yalihusisha mafunzo kwa vitendo ambapo washiriki walikwenda kujifunza namna ya kuhifadhi vyakula kwa njia za asili, kupika vyakula vya kiasili na ngoma ya Vanga na kuona ni namna gani ujuzi huo unarithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Tanzania ni mwanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa UNESCO wa mwaka 2003 unaolenga pamoja na mambo mengine kulinda utamaduni usioshikika kama lugha, mila na desturi pamoja na mambo mengine mengi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Super Eagles drop eight places in lastest...
Nigeria’s Super Eagles dropped eight places in the latest monthly...
Read more
Wizkid shares his thoughts as Davido gears...
Davido, the Nigerian music sensation, has just made a thrilling...
Read more
GARDNER GABRIEL ABASH TANZANIAN PRESENTER WHO DIED...
CELEBRITIES At 51, Captain Gardner G Abash is leaving the...
Read more
How to handle your wife during her...
Buy her what she craves for, chocolates, ice cream, her...
Read more
Pep Guardiola was heavily linked with the...
The appointment of Thomas Tuchel as England manager has led...
Read more

Leave a Reply