Kwanini Serikali Imelifunga Kanisa la Kiboko ya Wachawi?

0:00

5 / 100

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeagiza kufungwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, Temeke – Dar es Salaam baada ya kanisa hilo kwenda kinyume cha taratibu za usajili.

Barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 imewaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dominique Kashoix Dibwe kufunga tawi la Kanisa hilo linaloendeshwa na mchungaji huyo.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa za kufungwa kwake ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika jamii na mahubiri ambayo ni kinyume na maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.

Madai mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.

Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali imeagiza kufungwa Kanisa hilo, baadhi ya vitu kanisani hapo vimeondolewa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SERIKALI YAAGIZA MAMLAKA ZOTE KUHUSU UVUNAJI MAJI
HABARI KUU Serikali imeziagiza Mamlaka za Maji kushirikiana na Halmashauri...
Read more
ANAYEDAI KULAWITIWA NA ALIYEKUWA RC SIMIYU AMUOMBA...
Mwanafunzi wa moja ya vikuo vikuu jijini Mwanza, Tumsime Mathias...
Read more
IFAHAMU SIMU MPYA YA IPHONE 15...
Habari Kuu. Kampuni ya Apple ,hapo jana Septemba 12,2023 ilizindua...
Read more
SECRETS TO HAVING A STRONG RELATIONSHIP
If you desire a loving and lasting relationship with your...
Read more
KENYA NA TANZANIA ZAPIMANA UBAVU
HABARI KUU
See also  SHULE ZAFUNGWA SUDAN KUSINI KISA HIKI
Kufuatia maamuzi ya Mamlaka ya usafiri wa Anga...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply