Kwanini Msanii SNURA wa Majanga Amepiga Marufuku Nyimbo zake Kuchezwa Kwenye Vyombo vya Habari?

0:00

7 / 100

Mwanamuziki Snura Mushi ametangaza kuacha muziki huku akikataza nyimbo zake zisichezwe kwenye vyombo vya habari na sehemu nyingine, Hatua hiyo imekuja baada msanii huyo kudai kuwa kwa sasa ameamya kumrudia Mungu wake.

“Watanzania na nje ya nchi mimi Snura leo natangaza rasmi kuwa nimeacha kazi za sanaa nilizokuwa nazifanya. Sababu kubwa ya kuacha ni kumrudia muumba wangu, nifuate dini yangu ya Kiislamu inavyosema na mwanamke wa Kiislamu anavyotakiwa kuwa,” amesema Snura kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mbali na hilo, msanii huyo amesema anajutia aliyokuwa akiyafanya kipindi akiwa kwenye sanaa.

“Nisiwe muongo najutia sana niliyoyafanya na maamuzi yangu ya kuacha sanaa niliyafanya miaka mingi iliyopita, mwanzoni wazo langu lilikuwa kuacha kimyakimya nisiseme kwa yeyote wala popote ijue tu familia yangu, ndugu zangu na watu wanaonizunguka lakini kwa sababu hivi vitu vinaishi miaka na miaka na vizazi vipya vinakuja sitaki kuwa sababu ya kuwaharibu,” amesema.

Katika hatua hiyo ya kutangaza kuacha muziki pia ameomba nyimbo zake kuacha kuchezwa kwenye vyombo vya habari.

“Nisingeweza kupita kila redio na Tv kuwakataza wasicheze nyimbo zangu, natumia fursa hii ndugu zangu kwa heshima na taadhima naomba sana mnipokelee ombi langu msicheze kazi zangu kabisa naomba mfute, fanyeni kama hakuna kilichotokea,” amesema Snura.

Snura pia ameomba siku atakayofariki picha zake zisichapishwe kwenye mitandao ya kijamii.

“Ukisikia nimekufa umehuzunishwa na msiba wangu njoo unizike kama ni mwanamke usije mtupu njoo na stara, picha ambazo hazina heshima msiposti hayo mapicha wala madude dude kwa sababu naona tukifa hayo madude ndiyo mnaposti,” amesema.

See also  Mfahamu Didi-Stone mmoja wa watoto 7 wa Mwanamziki nguli Koffi Olomide

Baadhi ya ngoma alizowahi kutamba nazo Snura kabla ya kutangaza kuacha muziki ni ‘Majanga’, ‘Nimevurugwa’, ‘Chura’, ‘Shoga Yake Mama’, ‘Ushaharibu’ na ‘Shindu’.

Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa msanii kutangaza kuachana na kazi za sanaa na kumrudia Mungu. Mwaka 2016 mkali wa miondoko ya muziki wa taarabu, Mzee Yusuph alitangaza kuacha kazi za sanaa na kumtumikia Mungu. Hata hivyo mwaka 2020 alirudi tena kwenye kazi za sanaa alizokuwa akifanya awali.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

The National Assembly to Debate Inspector-General Nominee...
The National Assembly is set to deliberate on the Joint...
Read more
Khaby Lame will be a billionaire by...
Not because he's the most followed person on TikTok with...
Read more
Council of Legal Education Acknowledges Exam Result...
The Council of Legal Education has acknowledged a mix-up in...
Read more
THIAGO SILVA KUJIUNGA NA FLUMINESE
MICHEZO Nyota wa Chelsea, Thiago Silva mwenye umri wa miaka...
Read more
SEAN P DIDDY COMBS IS WILLING TO...
TRENDINGS So it appears that Sean P. Diddy combs is willing...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply