Tanzania leo Jumatatu Julai 29, 2024 imeanza vyema mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Paris 2024 baada ya mchezaji wake wa Judo, Andrew Thomas Mlugu (Uzito wa -73kg) kumtoa kwa Ippon (KO ya Judo) mpinzani wake William Tai Tin, kutoka nchini Samoa katika mchezo ambao Mlugu aliutawala toka mwanzo hadi mwisho.
Mlugu ndiye Mwafrika pekee aliyeshinda katika awamu hii kati ya jumla ya Waafrika wanne waliocheza leo.
Akiongea baada ya pambano hilo, Mlugu amesema pamoja na kumiliki na kushinda mchezo huo, lakini ameumia goti la kushoto wakati wa pambano. Hata hivyo amesema hatorudi nyuma bali ataendelea kupambana katika hatua inayofuata.
Katika Judo unaposhinda mpambano wa kwanza, unarudi tena mpambano wa pili ambapo mshindi anaingia robo fainali.
Ngwe inayofuata sasa Mlugu atapambana na Mfaransa Joan-Benjamin Gaba.
Katika Judo zege huwa halilali, kwa maana ya kwamba mapambano yanaendelea hadi mshindi wa kwanza apatikane.
Hii ina maana kwamba majira ya jioni ya leo washindi katika uzito anaocheza Mtanzania Andrew Thomas Mlugu watavalishwa medal za ushindi.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.