Wakili Boniface Mwabukusi ametangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwashinda Wanasheria wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo
Mwabukusi ameshinda kwa Kura 1,274 huku Sweetbert Nkuba akifuatia kwa Kura 807. Kwa matokeo hayo, Mwabukusi anakwenda kukiongoza Chama hicho cha Wanasheria kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mawakili wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo Kapt. Ibrahim Bendera aliyepata Kura 58, Paul Kaunda aliyepata Kura 51, Emmanuel Muga aliyepata Kura 18 na Revocatus Kuuli aliyepata Kura 7.
MATOKEO RASMI:
1. Boniface Mwabukusi kura 1,276 sawa 58%
2. Sweetbert Nkuba kura 807 sawa 36%
3. Ibrahim Bendera kura 58 sawa na 2.6%
4. Paul Kaunda kura 51 sawa na 2.3%
5. Emmanuel Muga kura 18 sawa 0.8%
6. Revicatus Kuuli kura 07 sawa 0.3%
Rais mpya wa TLS kwa mwaka 2024 hadi 2027 ni Wakili Msomi sana, Boniface Mwabukusi.