JESHI LA POLISI LAMTIA NGUVUNI ALIYESAMBAZA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU BINTI ALIEFANYIWA UDHALILISHAJI

0:00

5 / 100

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Amos Lutakulemberwa Lwiza mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Tegeta Wazo Kinondoni kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa binti anayedaiwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji amekutwa amefariki jambo ambalo ni uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Agosti 7, 2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa watu wajiepushe kusambaza taarifa za uongo kwani zimekua zikizusha taharuki ndani ya jamii.

“Jeshi la Polisi linatoa wito watu kujiepusha na kutoa au kuchapisha taarifa za uongo zenye malengo ya kuzusha taharuki katika jamii kwani kufanya hivyo ni makosa lakini litaendelea kuzingatia maoni ya watu ambayo hayakinzani na sheria za nchi”amesema SACP Muliro.

Akizungumzia kuhusu hali ya usalama kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba katika Uwanja wa Benjamini Mkapa SACP Muliro ameeleza kuwa Jeshi hilo limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.

“Usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu,hivyo tunawakumbusha nimarufuku kwa mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, watu watakaojihusisha na vitendo vyakihalifu ndani au nje ya uwanjawatashughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza SACP Muliro.

Mchezo wa soka wa watani wa jadi baina ya klabu ya Yanga na Simba zote za Dar es salaam utachezwa kesho kuanzia saa 1:00 jioni Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

See also  RAIS WA HUNGARY AJIUZULU WADHIFA WAKE
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WAZIRI MKUU AJIUNGA NA WANAWAKE KUANDAMANA ...
HABARI KUU Waziri Mkuu wa Iceland Katrin Jakobsdottir ,leo anaungana...
Read more
UGANDA YAZINDUA MFUMO WA KUZUIA RUSHWA
HABARI KUU Rais Yoweri Kaguta Museveni amezindua mfumo wa kielektroniki...
Read more
IMANI ZA KISHIRIKINA KUWACOST MUDATHIR NA FEISAL...
MAGAZETI Magazeti ya leo kwenye mbao za magazeti ya hivi...
Read more
HOW TO BUY COMPANY SHARES ON STOCK...
BUSINESS We will use Malawi as an example. Start by...
Read more
Raila Explains Reasons for Calling for Dialogue,...
Raila Odinga, the leader of the Azimio la Umoja -...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply