Mahakama ua Rufani imetupilia mbali shauri la maombi ya marejeo lilufunguliwa na mjane wa Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe wawili, ambao wamekuwa wakipambana kutetea wosia unaodaiwa kuandikwa na Mengi ambao mahakama kuu iliubatilisha.
Katika shauri hilo, Jacquiline na wanawe anaowasimamia, Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi walikuwa wanaiomba mahakama irejee na hatimaye itengue uamuzi uliotupilia mbali shauri la maombi ya mapitio waliloligu gua awali mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu, Iliyoukataa wosia huo.
Hata hivyo, katika shauri hilo la maombi ya marejeo namba 748/01 la mwaka 2022, mahakama hiyo katika uamuzo imewakatalia maombi ya kuurejea uamuzi huo ikisema sababu zilizotolewa hazina mashiko.
Katika uamuzi huo uliotolewa na jopo la majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, Rehema Mkuye (Kiongozi wa jopo), Abraham Mwampashi na Zainabu Muruke, mahakama imesema sababu walizozitoa si miongoni mwa zile za kuomba kufanya marejeo ya hukumu yake, bali zinahusu rufaa.
Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Muruke kwa niaba ya jopo hilo, ulitolewa Agosti 5,2025 na unapatikana katika tovuti ya mahakama iitwayo Tanzlii.