Polisi Yapiga Marufuku Maandamano na Mikusanyiko ya CHADEMA

0:00

7 / 100

Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina yoyote ile ya ndani au nje inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani kwa kuwa inalenga kuleta uvunjifu wa amani Mkoa wa Mbeya na maeneo mengine yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakihamasisha vijana kote nchini, viongozi wa kitaifa wa chama, kamati kuu ya chama hicho na kualika baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuadhimisha siku ya vijana Mkoani Mbeya huku wakitoa kauli zinazoashiria kuwa na lengo la kuvuruga amani.

Taarifa ya Jeshi la Polisi ya leo Agosti 11, 2024 imeeleza kuwa Miongoni mwa kauli hizo ni za Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa ndugu Twaha Mwaipaya, iliyosema “Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuweka hatma ya Taifa letu la Tanzania Mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanja wa Ruanda Nzovwe Mbeya”

Kauli nyingine ni, “Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, siku ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa serikali vijana wa kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025”

“Kauli zinazotamkwa kama hizi za kwamba wanakwenda kuamua hatma ya Taifa la Tanzania na kwamba wapo “serious” sana kama ambavyo vijana wa Kenya walijitambua na kuacha uteja wa serikali na taarifa zingine zilizopo ni viashiria tosha kuwa malengo yao sio kwenda kuadhimisha siku ya vijana duniani bali ni kuanzisha na kufanya vurugu ili kusababisha uvunjifu wa amani nchini.” imesema taarifa hiyo.

See also  SERIKALI YA NIGERIA YAFANIKIWA KUWARUDISHA MATEKA 137

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HUNTER BIDEN AKUTWA NA HATIA YA...
Hunter Biden (54), ambaye ni mtoto wa Rais wa Marekani...
Read more
AL AHLY KUIBEBA YANGA LEO USIKU? ...
MICHEZO Yanga inaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo...
Read more
President Ruto Touts Technical and Vocational Training...
President William Samoei Ruto emphasized the importance of equipping the...
Read more
MFAHAMU MOHAMMED DEIF "ROHO SABA" KIONGOZI WA...
NYOTA WETU Kamanda wa jeshi la HAMAS Mohammed Deif alitoa...
Read more
RUBEN AMORIM AKANA UVUMI WA KUJIUNGA NA...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Sporting CP, Ruben Amorim, amepuuzilia mbali...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply