Habari kutoka mkoani Dodoma zinaeleza kuwa
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu kwa jina la Mandojo amefariki duniani.
Taarifa ya awali zilizotolewa na mwanamuziki Domokaya ambaye pia waliwahi kuimba pamoja na mwingine Black Rhino zinasema Mandojo amefariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitalini baada ya kushambuliwa na kupigwa na watu waliodhani kuwa ni mwizi.
Wakati wa uhai wake Mandojo akiwa na Domokaya waliwahi kutamba na vibao kama
Nikupe Nini (2003), Dingi (2004) na Taswira (2005) ambayo walimshirikisha Inspekta Haroun.