Vyakula Vinavyosaidia Kuongeza Hamu ya Tendo la Ndoa Kwa Mwanamke

0:00

7 / 100

Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa (nyege) kwa wanawake ni miongoni mwa changamoto zinazoendelea kuwathiri wanawake wengi na hata kupelekea migogoro katika mahusiano au ndoa zao huku tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume likizidi kushika nafasi ya kwanza.

Zipo sababu nyingi zinazochangia tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na uzalishwaji mdogo wa homoni ya estrojeni katika mwili, matumizi ya dawa za kulevya, msongo wa mawazo (sonona), unywaji wa pombe.

Kwa kawaida wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa.

Inashauriwa kutumia vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu ya tendo la ndoa.Badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalumu.

Vyakula Vya Kuongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanawake:
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula vinavyosaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ambavyo ni pamoja na;

1) Spinachi.
Wataalamu wa afya wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mishipa ya damu inayozunguka viungo vya uzazi, uke. Damu inaposambaa vyema mwilini hasa kwenye viungo vya uzazi, uke hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka.

2) Pilipili.
Ndani ya pilipili kuna kompaundi iitwayo capsaicin ambayo hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo humuwezesha mwanamke kusisimka haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa.

See also  UKWELI KUHUSU UJENZI WA BARABARA MKOA WA MARA

3) Tangawizi.
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumika kwenye chai.

4) Asali.
Baadhi ya vitamini vinavyopatikana kwenye asali ni pamoja na ascorbic acid, pantothenic acid, niacin na riboflavin, madini yanayopatikana kwenye asali ni pamoja na calcium, copper, iron, magnesium, manganese, phosphorus, potassium na zinc. Vitamini na madini hayo husaidia katika uzalishaji wa homoni ya estrojeni na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

5) Parachichi.
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ni Parachichi. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kike. Inatajwa kuwa wanawake wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi.

6) Ndizi Mbivu.

Ndizi mbivu zina kiwango kikubwa cha potasiamu ambacho husaidia kuongeza uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kiume na kuboresha hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Tryptophan iliyopo ndani ya ndizi mbivu husaidia kuongeza utengenezaji wa serotonin, homoni inayoboresha hisia na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

7) Tikiti Maji.

Tikiti maji lina kiasi kikubwa cha asidi ya amino (L-citrulline) ambayo inachochea mtiririko wa damu kwenye uke. Wanawake wenye tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa wanaweza kunufaika kupitia L-citrulline kwa kula tikiti maji.

8) Karanga.
Karanga inasaidia kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Ongezeko la mzunguko wa damu kwenye uke humuwezesha mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kike.

9) Mbegu Za Maboga.
Mbegu za maboga zina phytosterol ambayo inajulikana kuboresha uzalishaji wa homoni ya kike, estrojeni katika mwili. Mbegu hizi pia zina mafuta yenye asidi ya omega-3 ambayo husaidia kuboresha mzunguko wa damu katika uke na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

10) Kitunguu Saumu.
Kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uke na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Hivyo unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika kila siku. Vile vile unaweza kutafuna punje 2 mpaka 3 za kitunguu swaumu kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata (chop) hizo punje 2 au 3 vipande vidogo vidogo kisha unywe na maji.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Napoli's narrow win over Genoa leaves Conte...
GENOA, Italy, 🇮🇹 - Napoli manager Antonio Conte was far...
Read more
Northeastern Elders Laud Duale's Reappointment as Defense...
Community Elders in Garissa County have welcomed the reappointment of...
Read more
Jurgen Klopp has distanced himself from taking...
Klopp, who left Liverpool at the end of last season...
Read more
Don't Marry A Stupid Man,Marry A Man...
Dear Ladies, DON'T MARRY A STUPID MAN,MARRY A MAN WITH...
Read more
RULES FOR GIRLS IN RELATIONSHIP
❤ Don't take off YOUR PANTIES because he called You...
Read more

Leave a Reply