Jeshi la polisi hapa nchini limekanusha kauli iliyotolewa na Aliyekuwa Kamanda wa polisi Dodoma Theopista Mallya dhidi ya binti anayedaiwa kubakwa na kulawitiwa kuwa “ni kama anajiuza”.
Jeshi la polisi kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo DCP David Misime imesema kuwa kauli hiyo sio msimamo wa jeshi la polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa kwa umma na jeshi hilo Agosti 4,6 na 9,2024. Na limeomba radhi kwa yeyote aliyeguswa au kuchukizwa na kauli hiyo.
“Tungependa kuwajulisha umma kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024” imeeleza taarifa hiyo.
Aidha Kamanda wa polisi Theopista Mallya amehamishwa kutoka mkoa wa Dodoma na kwenda makao makuu huku nafasi yake (RPC) ikichukuliwa na kamishna msaidizi SACP George Kitabazi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya amesema jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kwa ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es salaam limekamilika.
Vijana hao wanaodaiwa kutumwa na afande, wanne kati ya sita wameshakamatwa ambao walipanga na kutekeleza uhalifu huo. Tukio hilo liliibua mijadala mikali maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni.
Ukamataji huo umewagusa pia watu wengine wanane, kati yao wakiwemo wanne waliokamatwa kwa kukiua sheria na kusambaza picha mjongeo (video) za tukio hilo kwenye mitandao, zilizoonyesha ukatili huo.
Jana Agosti 18,2024 RPC wa Dodoma, Theopista Akizungumzia suala hilo na kinachoendelea kwa watuhumiwa hao, alisema katika uchunguzi wa jeshi la polisi ulibaini kuwa vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.
“Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu lakini yule dada alikuwa kama anajiuza ‘kahaba'”
“Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo. Alisema kamanda huyo.