Dar es salaam.
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani,Dkt Alex Malasusa amepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuwa Mkuu wa Kanisa akichukua nafasi ya Askofu Dkt Frederick Shoo aliyemaliza muda wake wa kikatiba.
Ameshinda kwa kupata kura 167 (sawa na 69.3%) akifuatiwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt Abednego Keshomshahara aliyepata kura 73 (30.3%).
Hiyo ni mara ya pili kwa Askofu Malasusa kuchaguliwa katika nafasi hiyo baada ya awali kuitumikia Mwaka 2007 hadi 2015 alipokabidhi majukumu kwa Askofu Dkt Frederick Shoo,ikumbukwe pia katiba ya Kanisa haizuii Askofu aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa kuchaguliwa kwa mara nyingine.
Tangu kuanzishwa kwa KKKT imeongozwa na wakuu wa kanisa wafuatao;
1. Askofu Dr .Stephano Moshi (1963-1976) kutoka Dayosisi ya Kaskazini
2.Askofu Dr Sebastian Kolowa (1976-1992) kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (Lushoto)
3.Askofu Dr .Samson Mushemba (1992-2007) kutoka Dayosisi ya Kaskazini Magharibi (Bukoba).
4. Askofu Dr. Alex Malasusa (2007-2015) kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
5.Askofu Dkt. FREDERICK SHOO (2015-2023) kutoka Dayosisi ya Kaskazini.
Katika uchaguzi wa leo majina ya Maaskofu watatu yamepitishwa na yamepigiwa kura kumpata Mkuu mpya wa Kanisa. Maaskofu hao ni;
1. Askofu Dr . Abednego Keshomshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Bukoba
2.Askofu Dr .George Mark Fihavango wa Dayosisi ya kusini, Njombe.
3.Askofu Dr Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Dr Malasusa amegombea huku ikikumbukwa mwaka 2019 jina Lake lilikatwa kwenye kinyang’anyiro hicho na uchaguzi wa leo umesimamiwa na Askofu Dr Amon Mwenda wa Dayosisi ya Ruvuma akiwa ndiye Mwenyekiti wa Uchaguzi.