Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameitaka serikali kukaa chini na wakazi wa Ngorongoro na kuona namna ya kumaliza changamoto zilizopo eneo hilo badala ya kutumia nguvu.
Mbali na hilo, Mbowe amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza wananchi wa Ngorongoro pamoja na kuwarejeshea huduma za kijamii.
Mbowe ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 22,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es salaam.
Kauli hiyo imekuja kutokana na maandamano yanayoendelea ya baadhi ya wakazi wa hifadhi ya Ngorongoro wanaopinga kinachotajwa kuwa ni kufutwa kwa vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo pamoja na kuondolewa kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za kiafya, vituo vya kupigia kura na mengine.
“Kuna Genocide/Uangamizaji mkubwa unaendelea Ngorongoro,haikubaliki kuwaondolea huduma za kibinadamu Wamaasai” amesema Freeman Mbowe
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.