Kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kubadilisha upendo kuwa chuki kwa wapendanao.
Na inawezekana tukawa tunayaona yakawaida Sana ila kiukwel sio yakawaida yakizidi.
- Ujuaji
Yaani unakuta mwanamke anajifanya mjuaji au anajiona ana akili za maisha kuliko mwanaume wake,kwa kawaida wanaume wanajiona kama kifaranga cha njiwa kisichoweza kupaa hivyo anakuchoka na atataka atafute mtu ambae atakuwa na sauti juu yake,hapa sio mwanaume anakukinai bali anakuchoka. - LAWAMA,NA KUMPANGIA NINI CHA KUFANYA
Inawezekana ni kweli mumeo ana matendo ya kukera sana lakini hupaswi kulaumu sana bali unatakiwa kutafuta njia ya kujenga kwa hekima.
Kikawaida wanaume wanatabia moja ambayo nahisi wanafanana.
Ukimshutumu kwa jambo Kama hafanyi ujue atafanya na hata kutengeneza mazingira uone anafanya,wanaume hawapendi mtu anaemkataza jambo kwa kulalamika yaan kila siku unaongelea jambo hilo hilo. - UBUNIFU
Ndio tunasema eti mwanaume hata umpe nini hawezi kutulia,kwanza hio nini ndio nini ?
Tuache kufata mkumbo kuna wanaume ambao hawajawahi kuchepuka na kuna waume ambao wanawajali Wanawake wao kama malkia ila shida ni kuwa watu wakifanyiwa vizuri huwa hawasemi ndio maana kila siku tunaona kero na vurugu kutoka kwa wanaume maana wanaofanyiwa vurugu ndio wanasema.
Sasa usijitume usijiwajibishe alafu ubaki kulaumu.
Na kuna ule usemi wa baadhi ya WANAWAKE wanasema mwanaume akikupenda hata usipojituma bado mtaishi vizuri ni kweli mtaishi vizuri lakini atatafuta pa kutimiza haja zake vizuri.
Kama unaweza panda dirishani uidondokee wewe dondokea,kama anataka style ya kusimama kama umepoteza matumaini na unaiweza wewe mpe si wa kwako bwana unataka apewe na nani ?
- KUMTEGEMEA KWA KILA KITU
Hapa namaanisha unaona bila yeye basi huna maisha,utataka upige kila muda na asipopokea unaleta vurugu,utume sms asipojibu basi shida,umuombe hela akisema hana basi unaleta shida.
My dear jifunze kujitegemea,kama umetuma sms na haja jibu acha kuwaza mabaya wewe tulia na ufanye mambo mengine.
Au umetuma sms tamu kakujibu kawaida unaona kama hupendwi.