Kauli tata za Rais Samia Suluhu

0:00

4 / 100

Jamhuri Ya Samaki…

Nimeisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri jana.

Nikiri sijawahi kumwona na kumsikia Rais Samia akiongea kwa namna ile.

Hotuba yake ilibeba ujumbe mzito ulioelekezwa kwenye anuani tatu, hivyo, hadhira tatu; wananchi wa kawaida, wanasiasa na Jumuiya ya Kimataifa.

Kwa andiko hili ningependa nijikite na anwani ya Wanasiasa na Wananchi.

Aidha, Rais Samia pia ni mahiri wa kufikisha ujumbe kwa njia ya fasihi. Kwenye fasihi kuna mawili yaliyojichomoza; samaki na muhali. Hilo la muhali pia nitalizungumzia kwenye andiko litakalofuata.

Ndio, na mashambulizi ya Samia kwenye anwani ya pili; wanasiasa, wala hakuyachelewesha.

“ Ukimya wangu si ujinga. Anayenyamaza kimya sio mjinga, na kupiga kelele si werevu.” Alitamka Rais Samia.

Kwamba kuna wanasiasa wameshasahau mapito waliyopitia. Si zamani sana. Kwamba hizo R4 wamezigeuza kuwa kichaka cha kufanya yasio ya taratibu.

Na sasa?

Rais wa Jamhuri ana taarifa nyingi.
Na hapa Rais Samia anazo taarifa na anawashukia wanasiasa hao kama mwewe;

“ Kumepangwa kushusha moto mpaka Samia aseme basi nimesarenda, naondoka. Hiyo Serikali au Serikali ya samaki?!”

Anaacha swali kwa hadhira yake ya kwanza; Wananchi.

Si ndio, kwa kauli hiyo ya Samia, basi, kuna ujumbe ameupeleka, kwamba ‘ The Lady is not for quitting.’
Kwamba Mama si wa kuachia ngazi na kuondoka.

Yumkini hao wenye kufikiri hivyo, Samia anawaambia Wananchi, kuwa wanasiasa hao hawamjui Samia.

Swali:

Jamhuri ya Samaki ikoje?

Jibu:

Ilivyo bahari ina samaki wa kila aina. Kuna nyangumi, papa, chewa, pweza, changu, ngisi na wengi wengine, bila kuwasahau dagaa.

Kwenye Jamhuri ya Samaki hakuna mifumo wala taratibu. Kila samaki anajiamulia vyake. Chewa atamla pweza, changu atamla kibua ili mradi ni vurugu tu baharini.

See also  Kwanini William Ruto amevunja Baraza la Mawaziri?

Na kuna samaki mdogo anaitwa kitakange. Wavuvi wa maji chumvi wanamjua vema samaki huyu mdogo lakini mwenye vurugu nyingi. Kitakange anaweza hata kuambaa baharini ubavuni mwa nyangumi bila hofu ya kumezwa.

Kitakange huyu ana sifa pia ya kuwachuza wenzake kwa maana ya kuwaponza hata samaki wakubwa baharini. Ni hivi, mvuvi anapotega gema baharini, gema lile lina matundu madogo madogo.

Samaki huyu kitakange huwavuta samaki wenzake na hata wale wakubwa hata wakaingia gemani. Wakati kitakange anapenya kwenye tundu za gema, samaki wenzake hubaki gemani. Hapo mvuvi huwafungia kirahisi.

Ni bahati mbaya, hata kwenye nchi yetu, tuna viongozi na wanasiasa wachache wenye tabia za samaki kitakange.

Nini Tafsiri yake?

Kimsingi mengine wayafanyayo baadhi ya wanasiasa ni ya kuturudisha nyuma. Ni misingi mizuri aliyoiweka Rais Samia ya R4 ambapo Maridhiano ni ‘ R’ Mama wa zote nyingine.

Kwamba yote yanazungumzika ili kupelekea mageuzi, uhimilivu na ujenzi mpya wa nchi. Hatukuwa nayo hayo, mpaka juzi tu, tulikuwa na watu waliokimbia nchi. Rais Samia anajenga misingi ya utawala wa Kidemokrasia, Haki na Sheria.

Ni ukweli, kuwa kama nchi, matukio yanayoendelea ya utekaji na mauaji yametuletea fadhaa na aibu kubwa. Yanaleta hofu. Yanaharibu taswira ya nchi yetu. Nchi tuliyozaliwa na tunayoipenda. Hatukuyazoea hayo. Ndio maana tuna lazima ya kulaani vitendo hivyo kwa sauti moja na kubwa.

Lakini, dawa ya kuyaondoa maovu hayo haiwezi kuwa kulifuta jeshi letu la polisi. Sote tuna wajibu wa kushiriki ulinzi wa pamoja kwa kujihami tukishiriana na polisi. Ndio tafsiri halisi ya falsafa yetu ya ulinzi jumuishi ya zama kwa zama- Total Defence.

See also  MAZITO ZIARA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA MKOA WA MARA

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA AFARIKI DUNIA
HABARI KUU Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Ngoyai...
Read more
NJIA HIZI 5 UTAMBULISHA MWANAMKE MALAYA
Makala Fupi Hivi ni viashiria vya Mwanamke ambaye hajatulia 1.SIO RAHISI...
Read more
Kenyan MP Ejected from Mombasa Resort Amid...
Dadaab Member of Parliament Farah Maalim has been removed from...
Read more
Leak private conversation between Nkechi Blessing and...
Nigerian Star actress Nkechi Blessing Sunday is relishing her blossoming...
Read more
WHAT TO DO WHEN YOUR SPOUSE HAS...
Several factors causes libido to peak or take a downward...
Read more

Leave a Reply