Muhimbili watoa orodha ya majeruhi ajali ya Kariakoo

0:00

4 / 100

Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa orodha ya majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo wakitokea ghorofa lililoporomoka Kariakoo.

Taarifa iliyochapishwa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma cha hospitali hiyo ya Muhimbili inaonesha kwamba imepokea majeruhi 40 waliopata ajali hadi kufikia saa 11 jioni.

Taarifa imesema 35 kati yao wameruhusia kwenda nyumbani baada ya kufanyiwa chunguzi na kubainika kuwa walipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa, kisha kuruhusiwa.

Watano kati yao bado wanaendelea na matibabu ambapo wanne wamepelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOl) kwa ajili matibabu zaidi.

Hata hivyo, taarifa hiyo imebainisha kuwa hospitali hiyo haijapokea maiti kutokana na ajali hiyo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Erik ten Hag aomba muda zaidi Manchester...
MICHEZO Erik ten Hag ameomba ‘uvumilivu’ baada ya kuthibitishwa kuwa...
Read more
KWANINI PAUL KAGAME ANAMHOFIA DIANE RWIGARA?
SIASA Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara ameondolewa kinyang’anyiro cha...
Read more
Kenyan MP Ejected from Mombasa Resort Amid...
Dadaab Member of Parliament Farah Maalim has been removed from...
Read more
Davido stirs uproar as he throws hot...
CELEBRITIES Popular singer, Davido sets tongues wagging as he throws...
Read more
Azam yanasa mbadala wa Fei Toto kutoka...
MICHEZO Klabu ya Azam FC imetangaza kufikia makubaliano na Klabu...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Waliomuua Mtoto Asimwe Wafikishwa Mahakamani

Leave a Reply