SABABU ZA KUCHEPUKA KWENYE MAHUSIANO au NDOA

0:00

Makala Fupi

Mahusiano au Ndoa hazikamiliki kwa kila kitu hata waliopo wangetumia muda gani katika kuchunguzana? Mwanzoni huwa ni rahisi kuingia kwasababu uwepo wa madhaifu unakuwa haupo . Kama ni mwanaume ataona pisikali na ataitongoza kwa ahadi kedekede na bashasha kubwa ,huku na hiyo pisi ikikubali kwasababu ahadi ni nzuri na za kuvutia.

Matatizo mengi, huanza pale Wapenzi wanapozoeana hasa katika hali fulani mathalani kwenye tendo la ndoa ndio huwa chanzo cha mambo yote iwapo mmoja atagundua madhaifu fulani ya mwenzake. Lakini pia hata kwenye mazungumzo ya kawaida, udhaifu unaweza pia kuwepo kwasababu kuna mwingine atamuona mwenzie kama akili haziko sawa nk.

HIZI NDIZO SABABU ZA WAPENZI KUCHEPUKA.

TAMAA ZA MWILI NA PESA

Ni jambo la kawaida kukosa na kupata kwenye utafutaji lakini kwasababu ya hali zetu za kimaisha kuwa tofauti basi wapenzi wetu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kuwa na mahusiano na watu wengine. Wanawake, siku hizi wana Vikoba ambavyo kila siku au wiki wanatakiwa kutoa hela. Sasa ikitokea,baba hujatoa hela ya kutosheleza basi Mwanamke anaweza kutoka nje ili apate mtu wa kumsaidia hili.

Wanaume pia unakuta kaoa Mwanamke mzuri lakini bado hatulii mpaka unajiuliza anatafuta nini? Lakini majibu ya wengi yamekuwa ni kutafuta ladha mpya. Kwa mtu,mwenye misingi mizuri ya maadili atailinda ndoa yake kwa gharama yoyote bila kujali hisia za mwili.

MADHAIFU KWA WAPENZI

Hali ya kimwili nayo inachangia pakubwa kwenye masuala ya mahusiano. Mfano mwanamume akishindwa kutekeleza majukumu ya ndoa yaani “hana nguvu za kiume” mara nyingi Mwanamke atashinikiza waachane ,kwa kuomba talaka na Mwanaume anaposhindwa kutoa basi Mwanamke analazimika kuchepuka bila ya hata kuwa mvumilivu.

See also  Jinsi Unyago na Jado zinavyosaidia Kukuza na Kuendeleza Maadili

Kwa upande mwingine, Mwanamke akiwa hapati UJAUZITO nayo inakuwa sababu ya mwanaume kutafuta Mwanamke wa pembeni hili apate uzao. Kwahiyo, kuchepuka kuna mambo mengi ambayo kwa Upande fulani yanaumiza waliopo kwenye mahusiano au ndoa zao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MBINU ZA KUACHA PUNYETO
Punyeto ni tabia kama zilivyo tabia nyingine kama kunywa pombe...
Read more
Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume
MAANA YA TEZI DUME: Tezi dume ni moja ya tezi la...
Read more
Ford Foundation Accused of Sponsoring Protests Violence...
The Ford Foundation, a prominent American non-governmental organization, has found...
Read more
SAUDIA ARABIA YAAMIA KWA WAAMUZI WA ULAYA...
Michezo Baada ya kuitikisa Ulaya kwa kusajili wachezaji nyota kwenye msimu...
Read more
ANTHONY JOSHUA ATAMBA KUMPIGA FRANCIS NGANNOU KWA...
MICHEZO Bondia Anthony Joshua ametamba kumpiga mpinzani wake Francis Ngannou...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply