Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa kwa maandalizi mazuri ya Kongamano la Uwekezaji mkoani humo litakaloibua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa mkoa.
Related Content
Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Desemba 19, 2024 mkoani Kagera wakati akizungumza katika Tamasha la Pili la Uwekezaji la mkoa huo ikiwa sehemu ya Wiki ya Ijuka Omuka (Kumbuka Nyumbani).
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa amesema chinbuko la Tamasha hilo ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeta ifanyike tathmini ili kujua sababu za kudorora kwa uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Kagera. Amesema mnamo mwaka 2022 wadau walikutana na kuainisha chanzo cha mkwamo kama mkoa.
Hata hivyo Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Kagera amehamasisha uwekezaji wa hoteli mkoani humo “Mikutano hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki haifanyiki hapa Kagera kwa sababu hatuna uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya watu, mfano Polisi kutoka nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walipenda kuja hapa kufanyia mkutano wao haikuwezekana kwa sababu hatuna ukumbi wa kuhifadhi watu 3,000 kwa pamoja hivyo walienda mahali pengine” amebainisha Mhe. Mwassa.
Related Content