Mbwana Samatta na Maisha Nje ya Soka

0:00

7 / 100

Mbwana Samatta, nahodha wa Taifa Stars na nyota wa PAOK Salonika huko Ugiriki, sio tu mchezaji wa kiwango cha juu bali pia ni mtu mwenye maono nje ya dimba.

Haya ni machache kuhusu alivyowekeza katika maisha yake ya baada ya soka.

Samatta, ambaye aliwika na Simba SC na TP Mazembe kabla ya kung’ara Ulaya na KRC Genk, ameonyesha upekee katika kujiandaa kwa maisha ya baada ya soka.

Taarifa na watu wa karibu wanasema kuwa amewekeza kwenye sekta ya majengo jijini Dar es Salaam.

Wanasema kila mwamba akimaliza jengo moja anaamia jengo jinyine.

Ameamua kujikita zaidi kwenye real estate business kwa ku-develop apartments kwa watu wa kawaida na commercial buildings.

Moja ya miradi yake ni majengo ya ghorofa yaliyopo Masaki, eneo la kifahari jijini Dar.

Ghorofa hizi zimejengwa kwa lengo la kupangisha, na ni sehemu ya mipango yake ya kuweka mizizi thabiti kwenye uchumi wa kisasa.

Licha ya mafanikio hayo, Samatta ni mtu wa kujichunga na media, hapendi kuweka wazi kila mradi wake wa kibiashara.

Chanzo cha karibu kinasema nyota huyu amewekeza pia katika miradi mingine ya kiuchumi na kimkakati lakini huweka mambo yake kama siri.

Smatta amewahi kujenga msikiti mkubwa sana lakini hakuna mtu aliyejua mpaka pale baba yake aliposema.

Ni moja ya watu maarufu wenye uwekezaji mkubwa kwenye real estate lakini hakuna anaejua ukubwa wa project zake na uwekezaji wake.

Hili ni somo kubwa kwa wanamichezo wetu – kuwekeza kwa busara si tu kwenye maduka ya nguo, bali hata kwenye real estate, ambayo ni sekta yenye fursa kubwa kwa sasa.

See also  SITI BINTI SAAD: JOHARI LA MUZIKI WA TAARABU ZANZIBAR

Mafanikio uwanjani yanaweza kuwa ya muda mfupi, lakini maono ya mbali kama ya Samatta yanatoa msingi wa maisha mazuri hata baada ya kustaafu soka.

Tunapaswa kuiga mfano wa nidhamu, bidii, na mipango thabiti ya Samatta kwa ajili ya kesho bora.

Haya ndiyo tunayotamani kuona kwa wanamichezo wetu wa Tanzania.

Tujifunze ili kuepuka hadithi za kusikitisha za wanamichezo wa zamani wanaohitaji misaada ya matibabu au wanaoishi maisha ya shida muda mfupi baada ya kustaafu.

Badala yake, tuwajenge wawe mifano ya kuigwa ndani na nje ya uwanja.

Samatta ameonyesha kuwa maisha ya mchezaji hayapaswi kuishia uwanjani.

Kwa muda mrefu, nimekuwa na ndoto ya kufanya kazi na wachezaji kama mshauri wa uwekezaji.

Wachezaji wanapata pesa nyingi sana lakini kwa bahati mbaya sio wasomi sana.

Lakini ukweli ni kwamba maisha yao ya soka ni mafupi mno.

Wanahitaji mtu wa kuwaongoza kufanya uwekezaji wenye manufaa ili kuwasaidia wakati wanaendelea na taaluma zao.

Wachezaji wa Ulaya ni kama taasisi; wana timu ya wataalamu wanasimamia fedha zao na kuzi-multiply kupitia uwekezaji wa kimkakati.

Cristiano Ronaldo amewekeza kwenye hoteli za Pestana duniani huku wachezaji wa Afrika wengi bado hawawekezi kwa kiwango kikubwa barani mwao.

Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Samatta na wachezaji wakubwa waliotambua kuwa soka ni la muda mfupi.

Namtakia Samatta kila la heri ndani na nje ya uwanja, nikiwa na imani kwamba uwekezaji wake wa kimkakati utamwandaa kuishi maisha bora baada ya kustaafu soka.

Huyu ni mfano halisi wa kwamba maisha yanaendelea hata baada ya mpira!

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

THE 12 RULES THAT WILL BETTER YOUR...
How can two walk together unless they agree? The truth...
Read more
Klabu ya Singida Black Stars (zamani Ihefu...
Patrick Aussems ni Kocha mwenye leseni ya UEFA PRO na...
Read more
Kalonzo Vows to Contest in 2027 Elections
Wiper party leader and Azimio la Umoja One Kenya principal,...
Read more
𝘽𝙪𝙨𝙞𝙣𝙚𝙨𝙨 𝙋𝙖𝙧𝙩𝙣𝙚𝙧𝙨𝙝𝙞𝙥𝙨; 𝙩𝙝𝙞𝙣𝙜𝙨 𝙮𝙤𝙪 𝙣𝙚𝙚𝙙 𝙩𝙤 𝙠𝙣𝙤𝙬...
For us to properly discuss partnerships, we must first define...
Read more
CAFCL ROBO FAINALI:YANGA VS MAMELODI,SIMBA VS AL...
MICHEZO Klabu ya Yanga SC itakutana na Klabu ya Mamelodi...
Read more

Leave a Reply