SIFA ZA MWANAUME BORA WA KUKUOA, KUWA MUMEO NI HIZI HAPA!

0:00

7 / 100

Wanawake wengi hulalamika kutokujua ni mwanaume gani anasifa za kumwoa. Wengi hawajua sifa za mwanaume mzuri atakayekuja kuwa Mume na Baba wa watoto wake. Sasa Binti yangu, Mimi kama Baba yako nikaona usiwe miongoni mwa walee wanawake wanaohangaika Kutafuta mwanaume Bora wa kuwaoa.

Ni Kweli unaweza Kuolewa, lakini je huyo atakayekuoa anasifa za kuwa Mwanaume mzuri, Bora na kuwa Baba kwa watoto wako? Hilo ndilo swali ka msingi.

Wanawake wengi wamejikuta kwenye mateso makali ya Kihisia na kimwili ndani ya ndoa. Kwa kushindwa kufanya uchaguzi sahihi wa mwanaume Bora. Wengine walifikiri Pesa pekee ndio kigezo muhimu cha mwanaume Bora baadaye walikuja kuumia pakubwa. Na ndipo wakajiunga na Ile Kwaya kubwa inayoimba, Bora Ugali Dagaa kwenye Amani kuliko Wali nyama Vitani.

Mimi Baba yako, Mtibeli, Mama yako akinichagua kwa Vigezo vifuatavyo ndio maana siku zote unamuona anafuraha. Nawe Binti yangu Fanya hivyohivyo;

  1. MWANAUME ANAYEJUA MWANAMKE ANAHITAJI NINI.
    Wanaume wengi husema huwezi kujua wanawake wanataka Jambo gani. Lakini ukweli ni kuwa wapo wanaume wanaojua
    Kile wanawake wanachohitaji. Na wanaume wote wanaojua kile wanachohitaji wanawake ndoa na familia zao huwa na furaha na Amani.

Usiolewe na mwanaume anayefikiri kuwa
Ninyi wanawake mnahitaji pesa kwa sababu huyo bado Hana uelewa wowote na ninyi Wanawake.
Mahitaji ya wanawake hubadilika badilika
Kulingana na wakati, Hali, mazingira, umri na matukio.
Mahitaji ya wanawake ni dynamic.

Moyo wa mwanamke umejengwa kwa nguzo kuu zifuatazo;

  1. Upendo.
    Hili ni hitaji lisilobadilika kwa mwanamke. Kila mara mwanamke atahakikisha anataka kuona unampenda, hata kama unampenda atazidi kuupima na kuujaribu upendo wa mwanaume ili kujihakikishia unampenda.

Kama mwanaume lazima ujue kumpenda Mkeo.
Mwanaume elewa, upendo kwa mwanamke pia hutokana na mtazamo wake na mila za jamii husika.
Kama upendo kwa sehemu unatokana na mtazamo wa mwanamke hii itamaanisha jinsi utakavyompenda mwanamke A ni tofauti na utakavyoweza mpenda mwanamke B.
Kwani mwanamke A huweza kutafsiri upendo kwa namna yake kulingana na Mtazamo wake ambao ni tofauti na mwanamke B.
Ndipo Ile kauli ya wanaosema Mapenzi hayana Kanuni au formula ndipo inapojitokeza.

Ni lazima mwanaume ajue mwanamke anamtazamo gani, akili yake inafanyaje Kazi, na amelelewa katika desturi na mila zipo.

  1. FARAJA.
    Mioyo ya wanawake ni rahisi kuvunjika, kuumia na kukatishwa tamaa. Mwanamke hahitaji utatuzi wa tatizo papohapo, yeye huhitaji FARAJA mara tuu Moyo wake unapovunjika au kuumia.
    Mfano, mwanamke anapokuelezea tatizo linalomsumbua au kumkera, hupaswi kutatua tatizo papohapo, unatakiwa umpe FARAJA Kwanza, mwambie Pole mke wangu, Onyesha kujali kwa kuwa karibu yake, mkumbatie.
See also  Vlahovic content to hear Juventus fan's jeers turn to cheers in Coppa win

Mfano amekuambia anajisikia kuumwa,
Usikimbilie Kununua Dawa au usikimbilie kwenda Hospital.
Mwite Mkeo, mkumbatie, awe kifuani mwako ahisi joto lako. Mguseguse kichwani na shingoni kama mtoto kuona kama anahoma, mpe Pole. Mueleze unavyompenda. Atahisi FARAJA kwa kuona unajali.
Utashangaa hata huko hospital au hata hizo dawa hatazihitaji.

Kwa nini? Kwa sababu, wakati mwingine wanawake humiss kudekezwa, kunakuwa(kupewa FARAJA) hivyo wakati mwingine hutengeneza matatizo ya uongo ili kutaka ukaribu wako, kuona jinsi unavyojali. Hivyo ndivyo kijana anatakiwa kufanya.

Sasa kijana usipokuwa na AKILI za kutosha, unaweza ukamtatulia Mkeo matatizo lakini bado akawa na kisirani na gubu. Unaanza kumlaumu. Oooh! Wanawake waajabu, unawatatulia matatizo Yao lakini hawana Shukrani wanakuwa na kisirani.

Hujawaelewa. Kuna Women Languages, women psychology.

  1. SIFA
    Wanawake hufanya kila Jambo na wanahitaji kusifiwa. Moyo wa mwanamke unanguzo Moja kubwa ya sifa. Mwanamke ili awe na furaha lazima umsifie.
    Njia Bora ya kumfanya Mkeo atie juhudi kukufurahisha hapo nyumbani kwako ni kumpa sifa.
    Sifa huongeza Ari na juhudi ya mwanamke kufanya vizuri zaidi ili kukufurahisha ili naye afurahie ndoa na mahusiano yenu.
    Ili Mkeo ajue kupika chakula kizuri sifia mapishi yake. Utashangaa ana-improve siku baada ya siku.
    Ili Mkeo akupe yote ajipindue, ajinyonge, akupe Mpaka ukomo wakati wa Sex msifie. Eleza jinsi alivyomtamu, eleza jinsi alivyo na joto, eleza jinsi alivyomlaini, eleza jinsi anavyojua kunyumbulika, eleza jinsi anavyokunja uso wake na anavyokudatisha.
    Siku kwa Siku utashangaa anazidi kuwa fundi na kukupa vitu na yeye anajifunza na kukazana zaidi.

Ni lazima mwanaume atakayekuoa ajue nguzo hizo.

  1. ZAWADI
    Moyo wa mwanamke umejengwa kwa nguzo ya ZAWADI. Hata kama zawadi ni ndogo kiasi gani. ZAWADI ni ishara ya kujali na kumkumbuka mtu ukiwa mbali naye.
    Elewa, Mkeo ili aliwe Nje wahuni wanatembea na hizi nguzo ili kuungusha moyo wake.
  2. MWANAUME ANAYEFANYA KAZI NA ATAKAYETAKA WEWE UFANYE KAZI.
    Mwanaume lazima akuulize unajishughulisha na nini kama wewe unavyomuuliza anafanya Kazi gani.
    Mwanaume anayetaka wewe ufanye Kazi huyo anataka upendo wa kweli kutoka kwako kwa maana mwanamke anayefanya Kazi na anakipato hawezi ku-fake upendo tofauti na Yule aliyefanya Kazi ambaye mara nyingi hutafuta mahusiano kwaajili ya Kupata wakumlisha. Mahusiano kama Ajira.

Watibeli tunaoa wanawake wanaofanya Kazi iwe ya kujiajiri au kuajiriwa. Ili kuepuka unafiki wa Wanawake.

Mwanaume ambaye hataki ufanye Kazi huyo hafai kuwa Mumeo hata angekuwa ni tajiri namba Moja duniani. Huyo anataka umuabudu, anataka uwe tegemezi kwake. Na hakuna mwanaume mwenye akili zake timamu, anayekupenda ambaye atataka usifanye Kazi.

Ikitokea Mwanaume akakuambia usifanye Kazi, akupe mbadala wa wewe KUTOKUFANYA Kazi mathalani, akununulie Hisa kwenye makampuni makubwa, ili uwe unapata faida kila mwaka.
Au akupe mradi kama nyumba ya kupanga na uwe kwa jina lako wewe uwe unachukua Kodi.

See also  Man United are better with Rushford says Amorim

Lazima nawe uwe na mchango ndani ya familia. Nazungumzia mchango wa kiuchumi hata kama kidogo. Yaani Ile mchango ambao ungekuwa upo mwenyewe ungeishije ndio uutoe ndani ya Familia yako kama Mke.

Ndoa haiwezi kuwa na furaha kama Mmoja wenu hafanyi Kazi. Ndoa haiwezi kuwa na furaha kama Mmoja wenu ni tegemezi.
Hakunaga mapenzi ya kweli ikiwa Mmoja ni tegemezi complete.
Lazima Mmoja atakuwa mungumtu mwingine mtumwa.

  1. UTU KWA WENGINE
    Mwanaume atakayekuoa lazima awe na utu kwa watu wengine wanaomzunguka. UTU kwa ndugu zake,
    Awe na mahusiano mazuri na ajue kutoa Haki kulingana na HAKI inayomstahili Mtu.
  2. AKUFANYE WEWE NI NAMBA MOJA.
    Kabla hajakuoa mwanaume Hakikisha umempima na Kupata Majibu wewe nafasi yako ni ipi kwake. Lazima uwe namba Moja kwake.
    Mwanaume ambaye hatakufanya namba Moja huyo hawezi kuifanya namba Moja familia mtakayoenda kuianzisha.

Mwanaume yeyote anayetanguliza wazazi au ndugu zake huyo hafai kuwa Mumeo. Usimzalie watoto, usianzishe familia na yeye.
Mwambie akaoe ndugu zake huko kwao.
Usimuonee huruma Wala usisikilize lolote kutoka kwake.
Wala usijidanganye atabadilika, hutakiwa kumbadilisha mtu hiyo sio Kazi yako.

Tafuta mwanaume anayejua maana ya Mke, huyo anajua maana ya Yeye kuitwa mwanaume na Mume.

Binti yangu, ni Bora usiolewe kabisa kuliko kuingia kwenye ndoa au kuanzisha familia na mwanaume anayetanguliza wazazi au ndugu zake. Bora ubaki single daima. Mimi Baba yako nitakuelewa.

Wanaume wanaotanguliza wazazi au ndugu zao kiasili hawapo kwaajili ya Kuanzisha familia zao. Wao wapo kwaajili ya familia za watu wengine.
Ni watumwa wa familia za watu wengine.

Hatukatai Wazazi na ndugu ni muhimu lakini haimaanishi wachukue nafasi ya MKE.

Vivyohivyo, kwa vijana, usikubali kuoa mwanamke anayetanguliza wazazi na ndugu zake. Huyo sio Mke wako. Mwambie akaolewe na wazazi au ndugu zake huko. Usimwonee huruma, usitumie Muda wako kumfundisha kuwa Mke. Hilo sio jukumu Lako.

Kuwa Mke/Mume ni Jambo la asili, natural mtu hujikuta hivyo. Sasa usimfundishe mtu kuwa Mke/Mume. Nia itakusumbua.

Mwanaume ambaye hajakuweka namba Moja huyo upo kwake kama geresha tuu. Hawezi ku- sacrifice kwa lolote kuhusu familia yake.
Huyo hajui na hajielewi anafanya nini kama mwanaume. Hajui kwa nini ameoa. Hajui kwa nini anaitwa Baba.
Anashindwa akili hata na wanyama kama Simba na kina Fisi.

  1. MWANAUME AMBAYE ATAKUSHIRIKISHA MAMBO KWA ASILIMIA 80%
    Binti yangu, huwezi kujiita Mchumba au Mke wa mtu ikiwa unaishi kama housegirl hapo nyumbani. Hujui nyumba hiyo mwaka huu mtafanya nini, yaani mnajiendea hata Wanyama hawafanyi hivyo.
    Lazima mkae kama Mke na Mume mpange kwa pamoja lakini Mume ndiye awe kiongozi wa familia yenu.
    Mwaka unaoanza tutanunua Moja, mbili, Tatu, kwa sababu Moja mbili Tatu
    Kipato chetu ni kiasi hiki kwa Mwezi.
    Itatupasa kila mwezi tutunze kiasi hiki.
    Mpaka mwezi wa sita vitu hivi viwili tuwe tumekamilisha.
    Tunahitajika kuongeza kipato kwa kufungua mradi au miradi mingine ili mambo yetu yaende kwa haraka.
See also  Marc Lasry nears purchase of NWSL's courage at $108m Valuation

Ndio mambo ya kuzungumza hayo sio unakuwa kama Housegirl kila siku kuulizia pesa ya kula anayoacha Mumeo. Ndio maana umaskini hautaisha kwenye familia na ukoo wako.
Housegirl ndiye huuliza maswali ya namna hiyo,

Na hauwezi ukakaa kwenye kikao cha mipango na malengo ya kifamilia na maendeleo wakati wewe hufanyi Kazi ya uzalishaji. Huna unachochangia chochote. Utasema mawazo au ushauri hivi kwaakili yako mawazo yako yatasaidia nini kwenye maendeleo,
Kama mawazo ya wanawake yangekuwa yanaleta maendeleo kwa wanaume Basi wanaume ambao hawajaoa wasingekuwa na maendeleo.

Linapokuja suala la maendeleo unasikilizwa endapo kuna nguvu na mchango Fulani utatoa na sio usikilizwe mawazo yako yasiyo na kichwa Wala miguu.

Kikawaida mawazo ya watu ambao hawafanyi Kazi za uzalishaji yanakuwaga utopia yaani mawazo ya abunuasi. Kwa sababu mtu anashauri Jambo asilo na uzoefu nalo. Tofauti na mtu anayefanya Kazi.

Zingatia, usitake mwanaume akushirikishe kwa asilimia Mia moja. Huyo haitakuwa Salama kwako
Na mwanaume mwenye akili na sifa ya kuwa Mume hawezi kukushirikisha kwa asilimia Mia moja. Lakini angalau 70% -80% hivi.
Hizo nyingine muachie kwaajili ya ulinzi na usalama wa familia.

Mwanamke anatakiwa ajue kuna ulinzi na usalama Kwa kiwango kikubwa lakini asijue asilimia zote za usalama wa kiuchumi wa mumewe.

Wengi waliojua waliasi au kuungana na adui kumuangusha mumewe.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Austria back in business, says Arnautovic after...
Austria captain Marko Arnautovic said his side are playing like...
Read more
JACOB ZUMA IS BACK ON THE RUNNING...
BREAKING NEWS Former President Jacob Zuma's appeal in the Electoral...
Read more
Ruto Unveils New Cabinet Lineup, Retains Several...
President William Samoei Ruto has revealed his new Cabinet nominations,...
Read more
15 REASONS WHY YOU ARE HAVING MARITAL...
LOVE TIPS ❤ 1. TO TEST YOUR LOVEThe moment you...
Read more
MWANAUME AWAPA WANAWAKE WATANO UJAUZITO KWA MARA...
NYOTA WETU. Lizzyash Ashliegh ,ambaye ni chanzo cha kusambaa kwa...
Read more

Leave a Reply