Kwanini Wasanii wa Tanzania wanakwenda kupima Moyo?

0:00

4 / 100

Wasanii wameendelea kuchangamkia fursa ya kupima moyo bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan huku wakimpongeza Rais kwa kuwapa fursa hiyo.

Akizungumza wakati wa uchunguzi wa moyo kwa wasanii hao, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge amesema amefurahi kuona wasanii wanachangamkia fursa hiyo na kuwataka wengine kuendelea kujitokeza.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa fursa hii ya kuwapima wasaniii bure, hii ni kuhamasisha wananchi wote wawe na tabia ya kupima afya zao ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanachangia vifo vingi sana,” amesema.

Naye msanii kutoka lebo ya muziki ya WCB, Mbwana Yusufu maarufu kama Mbosso amemshukuru Rais Samia kwa fursa hiyo akisema yeye ana shida ya moyo na amekuwa akifanya vipimo mara kwa mara kujua maendeleo ya afya yake ya moyo.

“Binafsi najifahamu nina matatizo ya moyo na ninaendelea na matibabu madogo madogo, nimefanya vipimo na nimeonekana bado ninashida nitafanyiwa vipimo zaidi na wameahidi kutatua changamoto yangu,” amesema na kuongeza,

“Ninamshukuru sana Rais Samia kwa kutupa fursa hii, ninawaomba wasanii waje kujua kama wana changamoto ya moyo, wasiogope kwasababu hapa ni vipimo na ukigundulika una shida unapatiwa matibabu,” amesema.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana amewashukuru wasanii kwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Rais Samia, huku akimshukuru pia Dkt. Kisenge kwa kufanikisha upimaji huo.

“Tunamshukuru na kumpongeza sana Dk Kisenge kwa kuratibu zoezi hili maana wasanii wamekuwa wakija hapa JKCI, na nimeona Diamond akihamasisha wasanii wengi waje, na leo ameleta pia kundi la wasanii wa lebo yake,” amesema.

See also  Kwanini Mahakama imemfutia Donald Trump mashitaka yanayomkabili?

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Erik ten Hag aomba muda zaidi Manchester...
MICHEZO Erik ten Hag ameomba ‘uvumilivu’ baada ya kuthibitishwa kuwa...
Read more
JUDE BELLINGHAM KUKOSA MASHINDANO YA LIGI YA...
MICHEZO Kiungo wa England na timu ya Real Madrid ataukosa...
Read more
3 THINGS YOU CAN DO TO INCREASE...
The strategies we apply for daily sales isn't rocket science.Truth...
Read more

Leave a Reply