Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba kutakuwa na siku ya kitaifa ya maombolezo itakayofanyika tarehe 9 Januari. Huku akiwasishi Wamarekani kutembelea maeneo ya ibada ili “kutoa heshima” kwa rais aliyefariki.
Pia Biden aliamuru bendera kupeperushwa nusu mlingoti katika majengo yote ya umma na ya kijeshi kwa kipindi cha siku 30, kipindi kinachojumuisha kuapishwa kwa rais mteule Trump.
Carter alihudumu kwa muhula mmoja (1977 hadi 1981). Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100, na alikua Rais mstaafu mwenye umri mkubwa zaidi akiivuka rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Hayati George H.W. Bush aliyefariki Novemba 30, 2018 akiwa na miaka 94.
Kwa upande wake Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema pamoja na changamoto za kiuongozi alizokutana nazo Carter alipokuwa Rais lakini alifanya kila liwezekanalo kuhakikisha anazimaliza na kuzitatua kwa faida ya taifa hilo.