MBOWE na LISSU wasichafuliwe ,tutashindwa kuwanadi

0:00

4 / 100

Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mbeya Chance Mwaikambo ambaye amekuwa kiongozi katika nafasi mbalimbali, ametia nia ya kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ndani ya chama hicho.

Akizungumza kuhusu nia yake hiyo, Mwaikambo amesema nia yake pamoja na malengo mengine kadhaa ni kwenda kuwasemea wanachama ambao wamekuwa wakikosa taarifa kuu zinazoadhimiwa na chama ngazi ya taifa kuchelewa kuwafikia wanachama na kwa uzito tofauti.

Pia amesema wana CHADEMA wana misiba mbalimbali inayowakabili katika kupambania demokrasia na upatikanaji haki hapa nchi hivyo kuahidi kuwa msemaji wa wanachama kwenye mikutano mikuu ya taifa ndani ya chama hicho.

“Kwanza lililonisukuma kwakuwa nimekaa na wanachama kule chini nafahamu wanataka nini na nitazungumza kamati kuu, sababu ya pili nimekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali, hivyo ninaweza kuwashauri viongozi wenzangu wa kitaifa kutokana na uzoefu wangu, na jambo la tatu mambo mengi yanatokea kamati kuu kuja chini lakini yanachelewa sana kwahiyo viongozi wakuu wanakuwa na picha kubwa sana ya kwenda kuwaondoa hawa CCM madarakani lakini wanachama wanakuwa hawana hiyo picha, nitakapoingia kamati kuu kutanipa nafasi ya kushauri ili picha ile ya kamati kuu ianze kule chini (kwa wanachama)”, ameeleza Mwaikambo.

Pamoja na hayo Mwaikambo ambaye alishawahi kuwa mtia nia ya ubunge jimbo la Mbeya Vijijini mwaka 2015 na 2020, katibu wa CHADEMA jimbo la Mbeya vijijini na mwenyekiti wa kamati ya mafunzo CHADEMA kanda ya Nyasa, amewashauri wanachama wenzake kukosoa kwa staha wagombea mbalimbali waliotia nia ya kugombea akisema hakuna haja ya kutoleana lugha mbaya kwani taasisi ni moja (CHADEMA).

See also  WTA roundup: Coco Gauff, Iga Swiatek win openers in Riyadh

“Ndani ya chama chetu (CHADEMA) kuna viongozi kwa maana ya mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti bara, hawa watu ni icon (nembo) kubwa ndani ya Chama chetu, ninatamani sana kuwasihi ndugu zangu, wanachama na viongozi wenzangu tunapokuwa tunawanadi kulingana na jinsi unavyompenda mgombea wako tupunguze maneno makali kwa sababu huu ni uchaguzi wa ndani ya Chama na baada ya uchaguzi ndani ya Chama kuna chaguzi za kiserikali yamkini chama kikamwamini Mhe. Freeman Mbowe kuwa mgombea wetu kwenye nafasi yoyote au Tundu Lissu je tutasema nini tutakapoenda kuwanadi hawa watu endapo tutakuwa tunawachafuana kuwavunjia heshima zao hawa viongozi wa chama hiki!”, amehoji na kueleza Mwaikambo.

CHADEMA inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa Januari 21, 2025 ambapo watachaguliwa viongozi na wajumbe wa Chama na mabaraza yake ili kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu baadaye Oktoba 2025.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts đź“«

Dumfries rescues point for Dutch in 1-1...
BUDAPEST, - Denzel Dumfries headed a late equaliser for the...
Read more
Bukayo Saka on winning the Premier League...
"We’ve been close the last two years, we’re getting closer…...
Read more
Manchester City claim victory in legal challenge...
Manchester City claimed a partial victory over the Premier League...
Read more

Leave a Reply