Balozi MONZE afukuzwa kisa kuomba kunyolewa sehemu za siri

0:00

4 / 100

Rais wa Zambia amemfuta kazi Balozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini kwa utovu wa nidhamu, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amechukua uamuzi huo baada ya Baalizi Bi Mazuba Monze, kuripotiwa kutaka wafanyakazi wake wa kiume kumnyoa sehemu za siri.

Mwanadiplomasia huyo ambaye alikuwa akihudumu katika ubalozi wa Zambia mjini Pretoria ameripotiwa kutoa ombi lisilo la kawaida, na agizo lisilo la kawaida, Bi Mazuba anatajwa kuwataka wanyakazi kumnyoa sehemu zake za siri ambapo wafanyakazi hao walikataa, wakisema kuwa haikuwa sehemu ya majukumu yao kumnyoa balozi hasa sehemu za siri.

Balozi alichukulia kitendo hicho kuwa ni kutotii na hivyo kupelekea kuwafuta kazi wafanyakazi, hata hivyo baada ya ukimya wa muda mrefu wafanyakazi walikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kulifikisha suala hilo kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wakati madai kuhusu matakwa hayo yaliyoshangaza wengi ya Bi Monze yalipothibitishwa, Rais Hakainde Hichilema alimfuta kazi mara moja balozi huyo wakati huo huo ripoti nyingine zinasema kuwa madai dhidi ya Bi Monze yametiwa chumvi.

Gazeti la Maravi Post linaripoti kuwa raia wa Zambia anayeishi Afrika Kusini amejitokeza, akidai kuwa madai dhidi ya Bi Monze huenda yametiwa chumvi au kutungwa na wapinzani wake, Mtu huyo anadai kuwa kampeni ilizinduliwa dhidi ya Bi Monze, ikihusisha ripoti za uongo na uzushi, ambao hatimaye ulisababisha kufukuzwa kwake.

See also  SIRI NZITO KUHUSU DKT SLAA NA WENZAKE KUACHIWA

Wakati haya yote yakiendelea, bado inabakia kusuburiwa ni hatua gani zaidi zitachukuliwa na matokeo gani Bi Monze atakabiliana nayo, hata hivyo jambo moja ambalo ni hakika ni tukio hilo limeacha doa kwa sifa ya kidiplomasia ya Zambia na kuibua maswali juu ya mwenendo wa wawakilishi wake nje ya nchi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

WATANO WAFARIKI NA 15 WAJERUHIWA ARUSHA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
President Ruto Touts Technical and Vocational Training...
President William Samoei Ruto emphasized the importance of equipping the...
Read more
High Court Sentences Acting IG Gilbert Masengeli...
The High Court has imposed a six-month prison sentence on...
Read more
Why RHULANI MOKWENA leaves Sundowns 🍃
The final and official decision is yet to be made...
Read more

Leave a Reply