HAJI MANARA ampigia debe MBOWE Uenyekiti CHADEMA

0:00

4 / 100

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, Haji Manara , ameonesha hisia zake kwa Mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe , akieleza kuwa anatamani kuona Mbowe akiendelea kushika nafasi hiyo licha ya changamoto za kisiasa zinazokikumba chama hicho kuelekea uchaguzi wake wa ndani.

Manara, akizungumza kupitia mahojiano ya hivi karibuni ya Manara TV, ameeleza kuwa alitumia muda mrefu kutazama hotuba na majibu ya Mbowe kwenye mahojiano, huku akivutiwa na namna alivyoonesha busara na ukomavu wa kisiasa.

“Juzi nilikaa YouTube kwa saa mbili nikimwangalia Mbowe. Hotuba yake na namna alivyokuwa anajibu maswali, hata pale alipoprovokewa, ilinivutia sana. Mimi ukiniuliza, uchaguzi ukifanyika pale, ningetamani kuona Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti,” amesema Manara.

Pamoja na kumpongeza Tundu Lissu kwa kuwa mwanasiasa mzuri, Manara ameweka wazi kuwa Freeman Mbowe ni mmoja wa wanasiasa bora zaidi nchini Tanzania, akisisitiza kuwa busara zake ni muhimu kwa ustawi wa chama hicho na upinzani kwa ujumla.

Manara alisisitiza umuhimu wa upinzani thabiti kwa maendeleo ya taifa, akieleza kuwa chama chake cha CCM hakihitaji matusi bali changamoto zenye kujenga.

“Sisi CCM wa kisasa tunahitaji upinzani imara ili utukosoe, utupatie changamoto, na kuhakikisha miradi inatekelezwa. Hatuhitaji mtu aje na matusi. Tunataka upinzani imara ili viongozi wa serikali wasilale na kero za wananchi zitatuliwe,” ameeleza Manara.

Manara ameongeza kwa kusema kuwa anatarajia upinzani kuwa thabiti na hatimaye kufikia hatua ya kuimarika kiasi cha kuchukua nafasi ya kuongoza kwa ‘kipindi kifupi’ kabla ya CCM kurejea madarakani.

“Baada ya kama miaka 50 au 100 ijayo, upinzani ukiimarika, basi tunaweza kuwaambia wachukue walau miaka mitano, kisha waturudishie utawala wetu,” amesema kwa utani.

See also  Doubles shuttlers Goh Sze Fei-Nur Izzuddin Rumsani were in sizzling form as they knocked out top Indonesian pair to reach the Japan Open semi-finals.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

From outcast to Chelsea leader: how does...
Chelsea defender Marc Cucurella looked good for Spain in the...
Read more
WHY STRONG WIFE IS A POISON TO...
LOVE TIPS ❤ Congratulations on having a strong wife but...
Read more
Arsenal thump West Ham to go second,...
LONDON, - Back-in-form Arsenal completed a high-scoring day in the...
Read more
WHAT YOU NEED TO KNOW ABOUT KISSING
Kissing is not just meant for sex You can tell how...
Read more

Leave a Reply