Paul Kagame akanusha nchi yake kuliunga mkono kundi la M23

0:00

5 / 100

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesisitiza kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 wanaozua ghasia nchini DR Congo hawafadhiliwi na serikali yake kama inavyodaiwa.

Aidha, Rais Kagame ameeleza kuwa vita katika eneo la mashariki mwa Kongo vimekuwa vikiendelea kwa miaka mingi, na kuuliza ‘’Je watu hapa hawajui jinsi vita hivi vilivyoanza? Vita hivi vilianza miaka mingi iliyopita na haikutokana na Rwanda.’’

Pia, ameeleza kuwa hana cha kusema kwani vita hivi vilianzishwa na makundi yalikuwepo Kongo na labda baadhi yao wana asili ya Rwanda lakini walikuwa wamehamia Kongo tangu enzi za ukoloni.

Rais Kagame amesema kuwa ingawa viongozi wa Kongo wameonekana kukiri kuwa waasi hao ni Wakongo na cha kushangaza ni kuwa wanadai kuwa vita hivi vinaungwa mkono na Rwanda.

Hata hivyo amesisitiza kuwa wapiganaji hao hawakutoka Rwanda, bali ni historia ya makundi ya zamani ambayo yana mizizi yake tangu wakati wa ukoloni.

Kauli ya rais Kagame inajiri baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Masisi siku tatu zilizopita kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wakosoaji wa Rwanda wanaishutumu, kwa kuitumia M23 kupora madini kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kama vile dhahabu, cobalt na tantalum, ambayo hutumiwa kutengeneza simu za mkononi na betri za magari yanayotumia umeme.

Kwa mujibu wa kituo cha BBC, Mwezi uliopita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilisema inaishitaki Apple kwa matumizi yake ya madini ya damu, na kufanya kampuni kubwa ya teknolojia kusema kuwa imeacha kutafuta madini kutoka kwa nchi hizo mbili.

See also  The crisis derby: Problems grow for Man City and Man United ahead of Premier League game

Rwanda imekuwa ikikanusha kuwa mshirika wa usafirishaji wa madini haramu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

Preston's Osmajic may face ban after leaving...
The Football Association (FA) said it will look into allegations...
Read more
SHERIA YAPITISHWA KUWALINDA WAAMUZI ...
MICHEZO Bodi inayotunga na kusimamia sheria na kanuni za mchezo...
Read more
13 THINGS YOU WILL REALIZE WHEN YOU...
❤ 13 THINGS YOU WILL REALIZE WHEN YOU ARE MUCH...
Read more
PSG must not be ruled by emotions...
Paris St Germain will not need any motivation when they...
Read more

Leave a Reply