Michezo
Hassan Mwakinyo ameingia kwenye mzozo na promota wa pambano lake na Mnamibia katika siku ya mwisho ya kuingia ulingoni ni baada ya promota huyo kukiuka baadhi ya vitu.
Mwakinyo mwanzoni alipangwa apigane na Okwiri lakini baadae huyu bondia aliumia na ikapangwa sasa,aje bondia mwingine. Mwakinyo alikiri kwamba jambo hili lilikuwa sio poa lakini alikubali kubadilishwa kwa bondia.
Promota alivunja makubaliano, ni baada ya kupungukiwa pesa na kutaka kuungana na promota mwingine. Mwakinyo alifanya bidii na kuwasiliana na Promota wake na kumweleza kama atakuwa na mapungufu ya hela basi yeye atamuongezea . Mwakinyo alitoa hela yake mfukoni na kumuongezea Promota na maandalizi yakaendelea kama kawaida.
Tofauti ilikuja ,ni baada ya Mwakinyo wakati anaenda kupima uzito alikutana na yule promota ambaye inatajwa Mwakinyo hakutaka promota wake amhusishe. Hassan Mwakinyo, alishindwa kukubali huyo mtu awepo kwenye kupima uzito huku ikumbukwe tayari yeye alikuwa ametoa hela zake mfukoni kwaajili ya kuhakikisha pambano linakuwepo.
Baada ya kushindwa kuendelea kwasababu ya hasira basi Azam Media ambao ni warusha matangazo ya michezo nchini waliomba kukutana na Mwakinyo eneo la Don Bosco na kutatua mgogoro uliojitokeza siku ya mwisho ya kuingia ulingoni.
Mazungumzo ya Azam Media na Mwakinyo ambayo yamekuwa ya siri mpaka sasa,yamemfanya Hassan Mwakinyo kukubali hivi leo kuzichapa na mpinzani wake Mnamibia, Julius Indongo.