SAMUEL ETO’O AINGIA MATATANI CAMEROON DiscoverCars.com

0:00

Michezo

Nafasi ya Samuel Eto’o ipo mashakani kama Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Cameroon (FECAFOOT) kutokana na barua iliotumwa kwa shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) na maafisa wa mpira wa miguu kutoka nchini humo wakishinikiza Eto’o ajiuzulu kutokana na kashfa kadhaa ikiwemo ya kupanga matokeo.

Kundi hilo ambalo ni pamoja na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu wa kulipwa Pierre Semengue na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la nchi hiyo FECAFOOT, Henry Njalla Quan Junior kwa pamoja waliwasilisha barua kwa Rais wa Shirikisho la mpira Duniani (FIFA),Gianni Infantino na kwa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF Patrick Motsepe wakihoji ni kwanini Samuel Eto’o amesalia kuwa Rais wa Shirikisho la mpira Cameroon pamoja na kashfa zote hizi nje ya uwanja?

Mapema mwezi Agosti, Shirikisho la soka Afrika ( CAF) lilifungua uchunguzi wa mwenendo usiofaa wa Samuel Eto’o baada ya sauti ya Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea kusikika kwenye upangaji wa matokeo ambayo aliipinga vikali.

Akizungumzia rekodi hiyo kupitia Gazzetta del Sports;-

“Nilikuwa nikizungumza na rafiki ambaye anawekeza katika soka na anataka kuifanya timu yake kuwa miongoni mwa timu kubwa nchini Cameroon. Nilimkakikishia tu kwamba ningefanya kila kitu kuepusha makosa ya waamuzi dhidi yake”.

Sambamba na rekodi hiyo,barua hiyo inaangazia pia kesi ya ukwepaji wa kodi,tukio lililozua mjadala Kwenye kombe la Dunia nchini Qatar 2022 baada ya mchezo wa Brazil 🇧🇷 na Korea 🇰🇷 ambapo alimvaa na kumpiga mpiga picha sambamba na hilo pia mkataba wake wa udhamini na kampuni ya kubashiri ya 1XBET.

See also  YANGA YAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI

Barua hiyo imegusia tukio la Rais wa Shirikisho la mpira nchini Uhispania Luis Rubialles kujiuzulu nafasi yake kutokana na tukio la kumbusu mwanadada Jenny Hermoso kama hatua ambayo Eto’o a anatakiwa kuichukua huku ikishangazwa na hatua ya CAF na FIFA kukaa kimya pamoja na malalamiko ya wadau wa mpira wa miguu nchini Cameroon 🇨🇲.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading