0:00
Habari Kuu
Silivia Bongo Ondimba, Mke wa Rais aliefurushwa madarakani Ali Omar Bongo Ondimba ameshitakiwa kwa kosa la utakatishaji pesa ambapo ofisi ya mashtaka imeziagiza idara za usalama kumuweka chini ya ulinzi nyumbani kwake baada ya Mahakama kupokea mashtaka yanayomhusisha na Rushwa na ufisadi.
Ofisi hiyo imesema mashtaka mengine yanayomkabili mke wa kiongozi huyo aliyepinduliwa na jeshi Agosti 30,2023 ni pamoja na kupokea mali za wizi ,kughushi na kutumia nyaraka na mali zilizopatikana kwa kughushi.
Hatua hii inakuja siku chache baada ya mtoto mkubwa wa Ali Bongo ashitakiwe kwa makosa ya uhaini na ubadhirifu wa mali za umma ikiwa ni baada ya kufanyiwa upekuzi na kukutwa na mabegi ya mamilioni ya fedha.
Related Posts 📫
MEXICO CITY, - Bam Adebayo won an Olympic gold medal...
IS A CHANGE OF ENVIRONMENTPerhaps you two should consider stepping...
MAKALA
Jambo la kwanza la kuzingatia inapokuja suala la kuchagua...
Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim...
Kanisa Katoliki limepata viongozi wapya, baada ya viongozi wa awali...