SAUDIA ARABIA YAAMIA KWA WAAMUZI WA ULAYA

0:00

Michezo

Baada ya kuitikisa Ulaya kwa kusajili wachezaji nyota kwenye msimu huu ,sasa Ligi kuu ya Saudia Arabia inatarajia kuajiri waamuzi kutoka pia barani humo. Waamuzi kutoka England wanatazamwa kwa jicho sana.

Katika hatua ya kuendeleza ligi kuu ya Saudia Arabia, waamuzi kutoka nchi kama New Zealand, Paraguay 🇵🇾 na Argentina 🇦🇷 walitumika kwenye michezo maalum. Hata hivyo, Saudia Arabia pro League ,inalenga kutoa kandarasi za msimu mzima,zenye mshahara mnono kwa waamuzi kutoka barani Ulaya.

Kwa wastani,mwamuzi wa kiwango cha juu Ligi kuu England, hulipwa kati ya paundi 120,000 mpaka paundi 300,000 kwa mwaka,kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail.

Hivyo, Ligi kuu ya Saudia Arabia imelenga kutoa nyongeza kubwa ya mishahara na makato madogo ya kodi hili kuvutia waamuzi kwenye ligi hiyo maarufu kama Saudia Arabia pro League.

Mwezi April, Mwamuzi kutoka ligi kuu ya England, Michael Oliver, alilipwa takribani paundi 3,000 kuamua kwenye mchezo wa Al-Hilal na Al-Nassr ,ya Cristiano Ronaldo, ikitajwa kuwa zaidi ya kiasi anachoingiza kwenye mchezo mmoja kwenye ligi kuu ya England.

Hofu imetanda juu ya ligi hiyo pendwa Ulimwenguni kupoteza waamuzi bora ,huku vyombo mbalimbali vikiripoti kuwa ,uamuzi huo utapingwa vikali.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Timu zapigana vikumbo kumnasa Ashley Cole
MICHEZO Ashley Cole ameripotiwa kuwekwa kwenye mipango ya kupewa kazi...
Read more
Super Falcons’ striker Asisat Oshoala, reflects on...
Asisat Oshoala responded to Nigeria’s defeat against Spain, acknowledging that...
Read more
Sabalenka Used Last Year's Loss in the...
Aryna Sabalenka used last year's loss in the U.S. Open...
Read more
Toni Kroos atangaza kustaafu soka
MICHEZO
See also  Pochettino akerwa na kichapo kutoka kwa Arsenal
Kiungo kutoka nchini Ujerumani na Klabu ya Real Madrid...
Read more
Adekunle Gold celebrates with joy on daughter,...
Nigerian singer Adekunle Gold radiates joy as he shares the...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply