CHELSEA YAPATA PIGO LINGINE

0:00

Michezo

Nahodha wa klabu ya Chelsea, Reece James, amefungiwa mechi moja pamoja na pamoja na faini ya paundi 90k zaidi ya TZS 270 milioni, kwa kosa la matumizi ya lugha isiofaa michezoni kwa Afisa wa mechi baada ya mchezo wa Chelsea na Aston villa kuisha kwa Chelsea kukubali kichapo cha 1-0.

Mlinzi huyo wa pembeni alikiri makosa ,kwa kumtusi na kunena maneno machafu kwa Afisa wa mechi kwenye njia ya kuelekea vyumba vya kubadilisha nguo ,baada ya mchezo huo kutamatika.

Tukio hilo linalinganishwa na la Nahodha wa Liverpool, Virgil Van Dijk ,wakati alipomtusi mwamuzi, John Brooks, kufuatia kadi nyekundu dhidi ya Newcastle mwezi Agosti.

James,ambaye ni majeruhi ,hakuwa kwenye kikosi kilichoikabili Villa ,lakini aliripotiwa kwa mamlaka za soka England FA kufuatia tabia yake dhidi ya mwamuzi Jarred Garrett, ambaye alihusimamia mchezo huo kwenye dimba la Stamford Bridge, mnamo Septemba 24.

Marufuku hiyo ya James, ilitakiwa kutimia kwenye mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi,hata hivyo tatizo lake la misuli ya paja linamaanisha kwamba hatohusika kwenye mchezo huo.

James, anaweza kurejea uwanjani Oktoba 21,pindi Chelsea itakapoikabili Arsenal, baada ya mechi za kimataifa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

President Ruto Challenges Gen Z Protesters to...
In a speech delivered in Taita Taveta, President William Ruto...
Read more
Mambo 10 ya kisheria ya kuzingatia kabla...
Mambo 10 kisheria unapaswa kuzingatia kabla hujanunua gari kwa mtu....
Read more
GABRIEL MAGALHAES APATA MAJERAHA TIMU YA TAIFA...
MICHEZO Arsenal imetikiswa baada ya beki wake mahiri kabisa, Gabriel...
Read more
Police Nominee Vows to Fortify Parliament, Pledges...
In his testimony before the National Assembly Committee on Administration...
Read more
MWANASIASA WA UPINZANI AKUTWA AMEFARIKI ...
HABARI KUU.
See also  Siri yafichuka AZIZ KI kumvuta nyota huyu wa Simba kujiunga Yanga
Mwanaharakati wa Chama cha upinzani cha Citizens Coalition...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply