NYOTA WETU
Mlinzi binafsi wa nyota wa Misri 🇪🇬 Mohammed Salah ,amezungumzia kazi yake ya kumlinda nyota huyo kutokana na mengi ikiwemo vitisho.
Karim Abdou amesema ;-
“Sarah ni maarufu Duniani, lakini ni maarufu kupita kiasi nchini Misri kutokana na umahiri wake kwenye soka pamoja na kutoa misaada yenye thamani ya mamilioni kwenye nchi yake.
“Hatupendi kupokea zawadi kutoka kwa mashabiki, lakini ikiwa tutazichukuwa basi tunaangalia usalama wake hili zisimdhuru au kumuua “.
Mlinzi huyo ameeleza mengi kwenye mahojiano na podcast ya 5ASide.
“Huyu ni kama mzimu ,hawezi kuonekana ,kuna siku alienda kusali Msikitini,hakuna mtu aliyekuwa akijua anaishi pale ,mtu mmoja alimfuata na kuweka kwenye kundi la WhatsApp kuwa MO Sarah anaishi kwenye anuani hii.
“Baada ya muda mfupi tu,takribani watu 20,000 walifika na kujaa.
“Lakini aliposhinda Ligi ya Mabingwa Ulaya huu ndio ulikuwa wakati mgumu kuliko yote.
“Ilikuwa Eid na kulikuwa na maelfu ya watu ,alitakiwa kwenda mtaani kusali na wengine na ndio alikuwa ametoka kushinda Ligi ya Mabingwa kwahiyo kila mtu alitaka kupiga nae picha.
“Hakuweza hata kufungua mlango, tulijaribu kumtorosha kupitia mlango wa nyuma, lakini ilishindikana”.