BARCELONA NA REAL MADRID KWENYE VITA

0:00

MICHEZO

Klabu ya Barcelona ipo kwenye vita kali na Real Madrid kuwania saini ya mchezaji wa Manchester City, Julian Alvarez.

Barca wanalazimika kurejea sokoni baada ya Mshambuliaji wao ,Robert Lewandowski kupata majeraha na kupelekea kutetereka kwa safu yao ya ushambuliaji ,jambo ambalo limefanya kuamua kuelekeza nguvu zao zote kwa Mshambuliaji huyo wa Manchester City, Julian Alvarez.

Mabingwa hao watetezi wa ligi ya La Liga walifanikiwa kuinasa saini ya kinda wa Athletico PR, Vitor Roque kutoka Brazil kabla ya Mshambuliaji huyo kupata jeraha la kifundo cha mguu ,ambapo anatarajiwa kuwa fiti kabla ya kuhamia rasmi Barcelona, mwezi Januari.

Ingawa Vitor Roque anaweza kuwa mchezaji bora katika siku zijazo,klabu hiyo itahitaji mchezaji imara ambaye anaweza kusaidiana na Lewandowski anayeelekea ukingoni.

Mshindi huyo wa kombe la Dunia na Argentina, yuko katika kiwango cha hali ya juu msimu huu baada ya kupachika mabao 6 na kutoa msaada wa goli 5 katika mechi 13 za Manchester City kwenye mashindano yote,Manchester City inashiriki Ligi kuu ya England.

Hata hivyo, sio Barcelona wanaohitaji huduma ya Mshambuliaji huyo pekee mwenye umri wa miaka 23 ,kwani Real Madrid wamepanga kumsajili iwapo watakwama kumsajili Kylian Mbappe msimu ujao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Raila Expresses Confidence in Ruto's Broad-Based Government
ODM leader Raila Odinga has expressed confidence that President William...
Read more
UNYWAJI POMBE KWENYE NDEGE UNAVYOSABABISHA MAGONJWA...
Wanasayansi wameonya Watu wasinywe pombe kabla ya kulala kwenye ndege...
Read more
SIMBA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA
MICHEZO Timu ya Simba ipo kwenye vilabu 12 vitakavyofuzu kushiriki...
Read more
FAIDA ZA KUNYWA MAJI YENYE MCHANGANYIKO NA...
AFYA
See also  MFAHAMU MSANII AYRA STARR WA NIGERIA
Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa...
Read more
Rais Samia atoa ujumbe mzito kwa viongozi...
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo kwenye...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply