WAFANYA VURUGU UBUNGO

0:00

HABARI KUU

Wafanyabiashara wa soko la simu 2000 lililopo halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ,Dar es salaam mapema leo,Alhamisi Oktoba 19,2023 wameandamana sambamba na kufunga barabara wakishinikiza mamlaka za serikali kuwapatia taarifa rasmi kuhusu tetesi zilizokuwepo awali kuwa wanatakiwa kuhama kwenye eneo hilo ili kupisha karakana ya wakala wa mabasi yaendayo kwa kasi (DART).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamelazimika kuchukuwa maamuzi hayo baada ya hapo awali kutopata majibu ya kuridhisha kutoka kwenye mamlaka husika za Ubungo hasa kwa Diwani na meneja wa soko hilo.

Mkuu wa wilaya Ubungo ,Hashim Komba,aliyefika eneo hilo akiwa ameambatana na maafisa wa jeshi la polisi ,Viongozi wa halmashauri na Viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo ameeleza masikitiko yake kwa hatua iliochukuliwa na wafanyabiashara hao kwakuwa wamechukuwa maamuzi yasiyokuwa sahihi na yanayokiuka sheria.

Amesema taarifa hizo hazina uhalisia wowote kwakuwa hazijatoka kwenye mamlaka husika na kwamba suala hilo lingekuwepo au litakuwepo wafanyabiashara hao wangeshirikishwa kwa kufanya vikao rasmi na wamiliki wa soko hilo ambao ni wamiliki wa halmashauri ya Ubungo.

Katika hatua nyingine Komba ameagiza vijana waliokuwa wameshikiliwa awali na maafisa wa jeshi la polisi kutokana na maandamano hayo waachiliwe na kuendelea na shughuli zao ,sambamba na kutoa onyo kwa yeyote atakaeanzisha vurugu ,mgomo au maandamano bila kufuata taratibu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Dalili za mimba au ujauzito wa watoto...
Mimba ya mapacha ni hali ambapo mwanamke ana mimba inayobeba...
Read more
Viongozi 10 wa Nchi wenye Magari yenye...
MAKALA
See also  BOMOA BOMOA KUANZA APRILI 12 DAR ES SALAAM
Jambo la kwanza la kuzingatia inapokuja suala la kuchagua...
Read more
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza...
Kauli yake inafuatia baada ya Rais wa Marekani Joe Biden...
Read more
Siri yafichuka kikao cha Pochettino na Todd...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino amefichua alikuwa na...
Read more
STEPHANE AZIZ KI ASAINI MKATABA MPYA YANGA...
MICHEZO Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki amesaini...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply