WAKONGOMANI WALITAKA JESHI LA AFRIKA MASHARIKI KUONDOKA

0

0:00

HABARI KUU

Muungano wa vyama vya kiraia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 umefanya maandamano mjini Goma ukitaka kikosi cha pamoja cha Afrika Mashariki kuondoka Mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kushindwa kukabiliana na waasi wa M23.

Mwezi Novemba mwaka jana, Kenya 🇰🇪, Burundi 🇧🇮, Uganda 🇺🇬, na South Sudan 🇸🇸 zilituma wanajeshi wake DRC ,chini ya bendera ya jeshi la kikanda la Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EACRF) ,kujaribu kulipokonya silaha kundi hilo la waasi na kuleta amani.

M23 imeendeleza kuyashikilia maeneo ya miji na vijiji vya Kivu Kaskazini.

Watu saba waliuawa mapema mwezi huu katika eneo hili. Wiki iliopita,Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Patrick Muyaya aliithibitishia idhaa ya Kiswahili ya BBC kwamba serikali yake haitawapa tena kandarasi wanajeshi wa kikosi hicho cha Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EACRF).

Alisema wanajeshi wa Congo watafanya kazi nzuri kuliko EACRF ambao pia amesema wanatakiwa kuondoka mwezi Desemba.

Katika taarifa ya hivi karibuni Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema vikosi vyake vimejitolea kufanya kazi kwa bidii pamoja na Serikali ya Congo huku likitaja mafanikio makubwa hasa ya kuhakikisha wakimbizi wanarejea salama.

Goma pia imeshuhudia maandamano makubwa dhidi ya ujumbe wa umoja wa Mataifa nchini humo.

Zaidi ya watu milioni 6.2 wamelazimika kuondoka makwao Mashariki mwa nchi hiyo na wanaishi kwingine nchini DRC, na wengine milioni moja na wengine wametafuta hifadhi ndani ya Afrika, hii ni kulingana na takwimu za umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ZIARA YA MFALME KENYA YAIBUA MAZITO

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading