PAPA ATEUA MAPADRI HAWA KUWA MAASKOFU

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francisco amewateuwa mapadri wawili kuwa maaskofu kwenye majimbo mawili ya kikatoliki ya Njombe na Bukoba.

EUSEBIO KYANDO

Maaskofu hao wateule ni pamoja na; Padri Jovitus Mwijage kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba na Padri Eusebio Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe .

Katika taarifa iliochapishwa na Vatican inasema Papa Francisco amemteua Padri Eusebio Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa msimamizi wa kiroho wa jimbo hilo.

Jimbo Katoliki la Njombe limekuwa wazi kwa muda mrefu kufuatia kifo cha Mhashamu Askofu Alfred Maruma na kwa upande wa jimbo la Bukoba Mhashamu Askofu Desderius Rwoma alistaafu kwa mujibu wa sheria za kanisa katoliki.

JOVITUS MWIJAGE

Hii ni mara ya kwanza kwa kanisa katoliki kupata teuzi mbili za maaskofu kwa wakati mmoja kwa miaka ya hivi karibuni kutoka kwa Baba Mtakatifu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WHY SMALL BUSINESS FAIL
BUSINESS REASONS SMALL BUSINESSES FAIL. 1.. LACK OF DEMANDThis usually affects...
Read more
Six Lies Leaders Tell Themselves That Lead...
THE SIX LIES:. I DON’T NEED ADVICE. Every leader who crashed...
Read more
Kurasa za Magazeti ya Leo
Dar es salaam, TANZANIA 🇹🇿.
Read more
JOSE MOURINHO AMPA ONYO MIKEL ARTETA
MICHEZO Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea na Man Utd...
Read more
SUALA LA RAIS SAMIA KUTOA SADAKA YA...
HABARI KUU Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Amour Hamad Salehe,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kwanini Donald Trump ana Nafasi ya Kushinda Urais wa Marekani?

Leave a Reply